ASSAs

UMOJA WA ULAYA, UINGEREZA WAANZISHA MAJADILIANO MAKALI YA BAADA YA BREXIT

229
0
Share:

Umoja wa Ulaya na Uingereza zimezindua majadiliano makali ya wiki tano leo, kuhusu makubaliano yatakayoainisha uhusiano kati yao baada ya Uingereza kuondoka kwenye kanda hiyo.

Duru hii mpya ya majadiliano mjini Brussels ndiyo ya kwanza kufanyika ana kwa ana tangu janga la virusi vya corona liliposababisha kufungwa kwa shughuli za kila siku.

Kuna matumaini kwamba kuongeza kasi ya majadiliano hayo kutawezesha kupatikana na muafaka, baada ya vikao vilivyopita kwa njia ya vidio kuleta mafanikio kidogo sana.

Lakini hamaki imeongezeka katika siku za karibuni, huku waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson akisitiza siku ya Jumamosi, kwamba nchi yake iko tayari kukubali madhara ya kuondoka bila mkataba iwapo hakutakuwa na maelewano.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, pia amekaza msimamo wake kwa kuhoji iwapo kweli London inataka makubaliano.

(Visited 20 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us