ASSAs

SHINYANGA: WANAFUNZI 101 WAPATA UJAUZITO KIPINDI CHA MACHI-APRILI MWAKA HUU

757
0
Share:

Wanafunzi 101 mkoani Shinyanga wamepata ujauzito ndani ya mwezi mmoja kuanzia Machi hadi Aprili mwaka huu wakati wa likizo ya kujikinga na maambukizi ya Corona

Mbali na ujauzito, Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Haki za Wanawake na Watoto la KIVULINI, Yassin Ally amesema mkoa huo una kiwango kikubwa cha ndoa za utotoni ukifuatiwa na Tabora

Amesema, “Kwa mujibu wa taarifa za dawati la jinsia, Machi – Aprili wanafunzi 101 wameripotiwa kupata ujauzito, ambapo Halmashauri ya Shinyanga ina wanafunzi 26, Kishapu 25, Manispaa Shinyanga 20, Msalala 17 na Kahama 16”

Mkurugenzi wa Wilaya ya Shinyanga, Hoja Mahiba amesema Serikali itawachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobaInika kuwapa ujauzito wanafunzi hao

(Visited 133 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us