ASSAs

RUKWA: WATU 380 WAMENUSURIKA KUFA BAADA YA MAJI YA KISIMA KUWEKEWA SUMU

397
0
Share:

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Justine Masejo amesema wanawashikilia watu wawili ambao wanatuhumiwa kuweka sumu katika kisima cha mfugaji Elias Juma wa kijiji cha Mkusa, Kata ya Kilangawana

Walionusurika kufa ni waombolezaji waliokuwa kwenye msiba huo karibu na kisima hicho na inaelezwa kuwa kabla ya kuanza kuyatumia maji hayo, walichotewa mifugo na walipokunywa walikufa papo hapo

Maji ya kisima hicho ndio yangetumika na waombolezaji kupikia na kunywa. Juma akieleza tukio hilo amesema amepata hasara kwani ng’ombe wa kisasa 16, Bata, Punda na Paka waliokunywa maji hayo walifariki papo hapo

Maafisa wa Polisi na mtaalamu wa afya walifika kijijini hapo na kufanya uchunguzi wa kitaalamu na kubaini kuwa mifugo hiyo ilikunywa maji yenye sumu ambayo haikuweza kufahamika mara moja

(Visited 104 times, 1 visits today)
Share this post