ASSAs

WANAOTANGAZA NIA YA KUGOMBEA MAPEMA WAPEWA ONYO KALI

171
0
Share:

Chama cha Mapinduzi ( CCM ) kimewaonya wanachama wake wanaochapisha mapango na vipeperushi kwenye karatasi au mitandaoni vyenye kuonyesha kuwa wanakusudia kugombea nafasi fulani kuacha mara moja kwani ni ukiukwaji wa taratibu.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchakato wa uteuzi wa Wagombea Urais, Katibu wa itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema kuwa mchakato wa kuchukua fomu za kuanza kugombea unaanza leo, hivyo wale wanaojitangaza wenyewe wamekiuka taratibu.

Aidha, ameziagiza kamati za maadili za chama hicho kwenye ngazi za kata, Wilaya na mikoa kuwakemea wale wote walioanza utaratibu huo mapema na wale watakaokaidi watashughulikiwa kwa namna nyingine.

(Visited 19 times, 1 visits today)
Share this post