ASSAs

JELA MAISHA KWA KUBAKA MTOTO WA MIAKA MITANO,KIGOMA

615
0
Share:

Jeremia Kilahunja (49) mkazi wa Katubuka amehukumiwa kifungo cha maisha baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka mtoto huyo tangu alipokuwa na miaka 6

Hakimu Mkazi wa Mahakama, Katoki Mwakitalu amesema Mahakama inatoa adhabu kali dhidi ya mshtakiwa huyo ili iwe fundisho kwake na kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo

Mshtakiwa huyo mara ya kwanza alimbaka mwanafunzi huyo akiwa na umri wa miaka 6 mwaka 2015, mara ya pili mwaka 2016, mara ya tatu mwaka 2017, mara ya nne mwaka 2018 na mara ya tano mwaka 2019

Mara ya 5 mshtakiwa alimkuta mwanafunzi huyo akiwa na mdogo wake wanachunga Mbuzi, alimuita na kumpeleka vichakani na kumbaka huku Mdogo wake aliyekuwa naye akiwachungulia

Walipofika nyumbani mdogo wa mwanafunzi huyo alimwambia mama yake tukio lililotokea wakati wakiwa wanachunga. Mama alimchukua mtoto na kupewa PF3 Polisi kwa uchunguzi na daktari alithibitisha mwanafunzi huyo hakuwa na bikira na ilionekana kufanyiwa kitendo kwa muda mrefu

(Visited 76 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us