ASSAs

TETESI ZA SOKA ULAYA: COUTINHO ANATUA ARSENAL, SANCHO HESABU ZIPO MANCHESTER UNITED

48
0
Share:

Chelsea inakaribia kukukubali maafikiano ya uhamisho na Bayer Leverkusen kwa mchezaji wa Ujerumani, 21, Kai Havertz. (Teamtalk)

Barcelona imemfanya mchezaji wa Manchester City, 19, raia wa Uhispania beki wa kati Eric Garcia mlengwa wao mkuu kipindi cha usajili kitakapofunguliwa msimu huu. (Goal.com)

Rais wa Napoli Aurelio De Laurentiis amesema kwamba beki wa kati wa Senegal Kalidou Koulibaly anaweza kuruhusiwa kuhama klabu hiyo ikiwa kiwango cha thamani yake cha pauni milioni 81 kitafikiwa. (Sky Italia, via Metro)

Mchezajki wa Borrusia Dortmund,Jadon Sancho

Kocha Ole Gunnar Solskjaer anataka Manchester United kuongeza kasi ya kumsaka mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Uingereza Jadon Sancho, 20, kuepuka hatua ya mvutano iliyojitokeza msimu uliopita kwa Harry Maguire. (ESPN)

Borussia Dortmund inaweza kujaribu kumsajili winga wa Uholanzi na aliyekuwa Manchester United Memphis Depay, 26, kutoka Lyon ikiwa United itamsajili Sancho. (Bild – in German)

Everton imetoa pauni milioni 18m kwa beki wa kushoto raia wa Uhispania wa Real Madrid, 23, Sergio Reguilon. (Sky Sports)

Arsenal wanafikiria kumtumia Matteo Guendouzi kama sehemu ya mpango wowote wa kubadilishana msimu huu
Maelezo ya picha,Mchezaji Matteo Guendouzi wa Arsenal

Kiungo wa kati wa Barcelona Philippe Coutinho, 28, amepata ofa ya Arsenal na Tottenham Hotspur, huku kukiwa na uwezekano wa Gunners kumsajili raia huyo wa Brazil na Barca ikipata pauni milioni 9 na kiungo wa kati wa Ufaransa Matteo Guendouzi, 21. (Independent)

Fulham, Bournemouth na Stoke City zote zinamnyapia mshambuliaji wa Uingereza, 21, Mallik Wilks, ambaye ndio amejiunga na Hull City kwa mkataba wa kudumu mwezi uliopita. (Football Insider)

Willian and Pedro

Barcelona na Inter Miami inayoongozwa na David Beckham zimetoa ofa ya mkataba kwa winga wa Chelsea raia wa Brazil Willian, 31. (Sky Sports)

Real Betis imeonesha nia ya kumsajili mlengwa wa Arsenal Dani Ceballos. Kiungo huyo wa kati, 23, yuko kwa mkopo Arsenal kutoka Real Madrid. (Onda Cero, via Sun)

Mshambuliaji wa Bournemouth Callum Wilson, 28, amewaambia wachezaji wenzake anataka kuondoka ili ajiunge na Ligi ya Premier kuendeleza matumaini yake ya Uingereza. (Telegraph)

Pierre-Emerick Aubameyang playing for Arsenal

Mshambuliaji wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang alikuwa tayari kuhamia Chelsea Januari lakini Blues ikashindwa kutimiza matakwa ya mchezaji huyo, 31. (Mailonline)

Manchester United itahitajika kufahamishwa ikiwa Borussia Dortmund itatoa kima cha kumsaka Depay kwasababu ya kipengee walichokiweka kwenye makubaliano wakati inamuuza raia huyo wa Uholanzi kwa Lyon. (Star)

Tanguy Ndombele and Jose Mourinho

Tottenham haiko tayari kumuuza kiungo wa kati wa Ufaransa Tanguy Ndombele, 23, licha ya Inter Milan kuonesha nia. (PA, via the42)

Beki wa kulia wa Uingereza Jeremy Ngakia, 19, anakaribia kujiunga na Watford kwa uhamisho bila malipo baada ya kuondoka West Ham. (Guardian)

(Visited 12 times, 1 visits today)
Share this post