ASSAs

UINGEREZA YAPIGA MARUFUKU KUTEMBELEANA MAJUMBANI KATIKA BAADHI YA MAENEO

49
0
Share:

Mamilioni ya watu kaskazini mwa Uingereza wanakabiliana na sheria mpya ya marufuku ya kutembeleana majumbani kufuatia ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona.

Sheria hiyo imeanza kutekelezwa mijini Manchester, mashariki ya Lancashire na sehemu ya magharibi mwa Yorkshire.

Katibu wa wizara ya afya ameiambia BBC kuhusu ongezeko la maambukizi kutokana na tabia ya watu kutembelea marafiki na ndugu.

Baadhi wamekosoa muda ambao tangazo hilo lilitangazwa kuwa majira ya jioni ya Alhamisi.

Katibu wa wizara ya afya bwana Matt Hancock alisema taarifa hiyo ililenga watu ambao walikuwa wamekutana na waliombukizwa kuacha kutembelea jamaa zao ili kupunguza maambukizi.

(Visited 9 times, 1 visits today)
Share this post