ASSAs

UJERUMANI ITAZIBA PENGO LA WANAJESHI WA MAREKANI

69
0
Share:

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani amesema leo kwamba atafanya mazungumzo baada ya kumalizika msimu wa joto na mawaziri wa majimbo ya Ujerumani yaliyoathirika kutokana na uamuzi wa Marekani wa kuondoa wanajeshi wake wapatao 12,000 nchini humo.

Annegret Kramp-Karrenbauer amesema watajadili jinsi wanajeshi wa Kijerumani watakavyoweza kuyasaidia maeneo yaliyoathirika na uamuzi huo. Ameongeza kwamba watazingatia masilahi ya Wajerumani na raia ya Ulaya, kwani maisha mazuri yanahitaji usalama.

Jeshi la Marekani Jumatano lilitangaza mipango yake ya kuwaondoa wanajeshi hao, kufuatia mvutano wa muda mrefu uliokuwa ukitokota kati ya Rais Donald Trump na viongozi wa Ujerumani.

Hata hivyo Marekani imesema kwamba nusu ya wanajeshi hao watabakia katika mataifa mengine ya barani Ulaya kushughulikia mvutano na Urusi.

(Visited 17 times, 1 visits today)
Share this post