ASSAs

WANAFUNZI BILLION 1 WATAADHIRIKA NA KUFUNGWA KWA SHULE

664
0
Share:

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema leo kuwa janga la virusi vya corona limesababisha mvurugiko mkubwa wa elimu katika historia, wakati shule zilifungwa katika zaidi ya nchi 160 katikati ya mwezi Julai, na kuwaathiri zaidi ya wanafunzi bilioni moja.

Pamoja na hayo, mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa alisema kiasi ya watoto milioni 40 duniani kote wamekosa elimu, katika mwaka wao muhimu wa kabla ya kuanza shule.

Kwa matokeo hayo, Guterres alionya kuwa dunia inakabiliwa na kizazi cha maafa ambacho kitapoteza uwezo mkubwa wa kiutu, na kuharibu miongo kadhaa ya maendeleo, na kuongeza hali iliyopo ya kutokuwapo na usawa.

Kwa mujibu wa makadirio ya shirika la UNESCO katika nchi 180 kiasi ya watoto milioni 23.8 wanahatari ya kuacha shule ama kutopata nafasi ya kuingia shule mwaka ujao kutokana na athari za kiuchumi kutokana na janga la virusi vya corona.

(Visited 97 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us