ASSAs

IDADI YA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA CORONA AFRICA YAFIKIA MILLION 1

299
0
Share:

Idadi ya maambukizi ya virusi vya corona barani Afrika imepindukia milioni moja. Nchi nyingi barana humo zinahofia kuzuka kwa wimbi la pili la maambukizi.

Kulingana na taarifa za shirika la habari la AFP mataifa ya barani Afrika kwa jumla yameorodhesha idadi ya watu1,011,495 waliomabukizwa virusi vya corona.

Idadi hiyo inawakilisha karibu asilimia tano ya maambukizi ulimwenguni kote. Jumla ya watu 22,115 wamefariki kutokana na virusi vya corona barani Afrika.

Taasisi ya bara la Afrika inayosimamia Vituo vya Kudhibiti magonjwa imesema nchi tano barani humo zimekumbwa na asilimia 75% ya maambukizi.

Shirika la Afya Ulimwenguni WHO limesema nchi kadhaa barani humo zinashuhudia kupungua kasi ya maambukizi kwa karibu asilimia 20 katika kila siku. WHO imesema nchi za Kiafrika zinafanya kila bidii, licha ya kuwa na mifumo dhaifu ya kiafya.

(Visited 22 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us