ASSAs

LISSU ATANGAZA VITA DHIDI YA WAMACHINGA TANZANIA. ASEMA, WAMEKUA KERO KWA WAFANYA BIASHARA WA KIGENI.

2708
0
Share:

(kutoka Tunduma Mbeya)

Anayetarajiwa kuwa Mgombea wa nafasi ya Urais kupitia tiketi ya CHADEMA ndugu Tundu A Lissu ameweka wazi msimamo wake juu ya Wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kama machinga. Machinga ni wale wote wanaofanya biashara ndogondogo wakiwa ni vijana, akinamama na wazee wachache.

Wengi wao mitaji yao inaanzia shilingi elfu moja hadi laki moja. Machinga wamekua wakifanya biashara kwa kuzunguka kutoka sehemu moja kwenda nyingine na wengine hutembea kwa umbali wa kilometa hadi 30 kwa mguu wakiwa na bidhaa zao mgongoni ama kichwani, bidhaa hizo nikama mayai,sindano za kushonea nguo pamoja na vitambaa vya kufutia jasho nk.

Wafanya biashara hawa wamekuwa wakiteseka sana kwa kuugua na jua na wakati mwingine kunyeshewa na mvua.
Mtakumbuka wafanya biashara hawa ni wale walioteseka sana kwa miaka ya nyuma kama kupigwa na migambo kunyang’anywa vitu vyao na kumwagiwa kabisa vitu vyao. Wamachinga waliwahi kuingia mgogoro na Serikali baada ya baadhi ya viongozi kuwapangia kufanya biashara katika maeneo yasiyo na mzunguko au mkusanyiko wa watu.

Tangu Mwaka 2015, Rais magufuli aliamua kutangaza kuwahurumia na kuwapa uhuru wa kufanya biashara mahala popote wanapotaka hata kama ni viunga vya Ofisi zote za umma kama vile kwa Mkuu wa mkoa au Wilaya bila kubughudhiwa na mtu yeyote. Rais Magufuli alitangaza kiama kwa yeyote atakaye wasumbua na kuwanyanyasa machinga.

Rais Magufuli aliongeza jukwaa la waliosamehewa kuwa ni kuanzia mwenye mtaji wa Milioni nne kushuka chini. Hali hii ilipeleka kuongezeka kwa watu waliopata msaada wa kufutiwa ushuru chonganishi na ushuru bugdha. Hivyo kwanzia Bodaboda,wauza vinjwaji, mama ntilie na machinga wote kiujumla walipewa uhuru wa kufanyabiashara zao. Rais Magufuli alitangaza kuwa ameamua kuwasamehe na kuwalinda Machinga kwasababu ndiyo waliompigia kura.

Rais aliamua kuagiza halmashauri zote kuhakikisha wanatoa ile asilimia kumi ya mapato na kuielekeza kwa Vijana, akina mama na walemavu kama sheria inavyotaka na Kiongozi ambaye katika eneo lake angeshindwa basi yeye angemtimua kazi. Wote hao ni Machinga.

Rais Magufuli aliamua kuanzisha vitambulisho vya machinga tena kwa gharama za Serikali ili Machinga Watambulike Rasmi na wao kutambuana ili wasisingiziwe kwamba wao ni wazururaji wasio na kazi kama ilivyofanyika hapo awali. Leo Machinga wamekuwa na thamani kubwa na kuwa wenye tija kwa taifa. Wamekuza biashara na kuongeza soko la ajira na viwanda nchini.

Leo machinga wanaheshimika na kutoonekana vibaka kama hapo awali bali watuwenye mchango mkubwa katika jamii. Leo machinga wamekua na vikundi vyao rasmi ambavyo wanavitumia kusaidiana katika shida na raha kwenye masuala ya kiuchumi na kitamaduni.

Msimamo wa Tundu Lissu na CHADEMA juu ya Machinga Tanzania. Lissu Ametangaza kiama kwa wamachinga katika siku 100 za mwanzo endapo atakua amepata Urais. Lissu ameenda mbali zaidi kwa kusema akiingia madarakani atafuta vitambulisho vya machinga na hakutakua tena na urasmi wa machinga. Hii ni kwamba taifa litarudi tena kwenye mgogoro na Machinga kama hapo awali.

Machinga wengi watapoteza ajira zao na mitaji. Kwakua hakutakua na kutambulika tena Machinga wataitwa wazururaji, vibaka na wasio na kazi hapo awali. Lissu anawaona Machinga kama tatizo kwasababu hawaungi mkono harakati zake.

Kutangazwa kwa vita ya Lissu dhidi ya Wamachinga kumefanywa na Lissu mwenyewe kwa kushawishiwa na baadhi ya wafanyabiashara wakigeni Waliompakani Tunduma. Mbele ya Wafanyabiashara wakubwa wa kigeni mpakani Tunduma amaboa waliahidi kumsaidia katika harakati za kupata urais Lissu kwashart la kuondoa urasmi wa Machinga kwani wamekuwa kero kwa wafanya biashara hao, Lissu aliwaahidi kuwa atafuta vitambulisho ili Umachinga usiwe rasmi nchini.

Na alipokenda kwenye mkutano wa hadhara alitangaza kufuta vitambulisho hivyo.Hali hii imezua hofu kwa Wamachinga mwenyeji kuona kwamba siku zao zinahesabika. Wamachinga wanaona kuwa watakuwa na wakati mgumu sana endapo Lissu atakuwa Rais kwani watakimbizwa na kupigwa na migambo kama hapo awali na kupoteza biashara zao ukizingatia wengi wanalea na kusaidia familia zao kupitia biashara hizo.

(Visited 825 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us