ASSAs

WAJUMBE CCM WAMKATAA MGOMBEA ALIETEULIWA WATANGAZA KUSHUSHA BENDERA ZA CHAMA CHAO

713
0
Share:

Katika hali isiyokuwa ya kawaida,baadhi ya viongozi na wajumbe wa Chama cha Mapinduzi CCM kata ya Mji Mwema mjini Njombe,wamesema wako tayari kwenda kushusha bendera za Chama chao na kuto shiriki shughuli za kampeni katika kata hiyo kupitia Chama cha Mapinduzi kutokana na kutoheshimiwa maamuzi yao.

Wajumbe wa Kata hiyo wamelazimika kuweka wazi uamuzi wao kutokana na juhudi zao za kuzunguka kwa zaidi ya siku mbili mfululizo ngazi zote zinazohusu uchaguzi ngazi ya kata bila mafanikio.Wamesema wanashangazwa mgombea wao Nestory Mahenge aliyeshinda kura za maoni kushindwa kuteuliwa badala yake kuletewa mgombea aliyeshika nafasi ya pili Ndugu,Abuu Mtamike aliyehamia katika Chama hicho akitokea Chama kikuu cha Upinzani CHADEMA.

Hata hivyo wanasema kutokana na kuonyesha juhudi za malalamiko yao wamefanikiwa kukabidhiwa barua kutoka kwenye Chama chao lakini bado mpaka sasa wanasumbuliwa na kushindwa kupewa barua kutoka kwa msimamizi msaidizi wa Uchaguzi ngazi ya kata hiyo.

(Visited 211 times, 1 visits today)
Share this post