ASSAs

TETESI ZA SOKA ULAYA IJUMAA 28/8/2020 MESSI, REGUILON, HAVERTZ, IBRAHIMOVIC, RONALDO, DEENEY, DOHERTY

886
0
Share:
Messi

Mshambuliaji wa Argentina, Lionel Messi mwishoni mwa wiki amewasiliana na meneja wa Man City, Pep Guardiola na kumfahamisha kwamba anataka kuondoka Barcelona.

Manchester City inaweza kuwatoa mabeki wake raia wa Hispania Eric Garcia, 19, na Angelino, 23, kama chambo ili kumnasa Messi, kama hawatamsainisha akiwa mchezaji huru.

Manchester City inajiandaa kuipa Barcelona kitita cha £89.5m pamoja na Garcia, kiungo wa Kireno Bernardo Silva, 26, na mshambuliji wa Brazil Gabriel Jesus, 23, kwa ajili ya kumnasa Messi. (Sport – in Spanish)

Real Madrid inataka 20m euros kwa ajili ya beki wake wa kushoto wa Hispania Sergio Reguilon, 23 ambaye alivivutia vilabu vya Manchester United, Tottenham, Juventus na Inter Milan wakati akicheza kwa mkopo Sevilla. (Marca)

Chelsea iko katika hatua za mwish kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji wa Kijerumani anayekipigia Bayer Leverkusen, Kai Havertz. (Guardian)

Kai Havertz

Mshambuliaji wa zamani wa Sweden Zlatan Ibrahimovic, 38, amekubali mkataba mpya wa mwaka mmoja kusalia AC Milan, mkataba unaoaminika kuwa na thamani ya £6m. (Sky Sports Italia – in Italian)

Mshambuliaji wa Ureno, Cristiano Ronaldo, 35, amezima tetesi kuhusu mustakbali wake kwa kusema kwamba anajiandaa kwa msimu wa tatu Juventus. (Mundo Deportivo – in Spanish)

Mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann, 29 aliamua kuikacha Barcelona kabla ya kushawishiwa kubaki na Meneja mpya wa timu hiyo Ronald Koeman. (RMC Sport via Metro)

Antoine Griezman

Kuwasili kwa beki wa kulia Raia wa Ireland, 28 Matt Doherty katika timu ya Tottenham kutoka Wolves kunaweza kuwa tiketi ya mlinzi wa Ivory Coast, Serge Aurier, 27, kuondoka. (Standard)

Tottenham imekataa ofa ya kwanza kutoka AC Milan kwa ajili ya Serge Aurier, huku Bayer Leverkusen ikionyesha nia ya kutaka huduma ya mlinzi huyo. (Sky Sports)

Manchester United imewasilisha ombi la kumnasa kiungo wa Brescia Sandro Tonali, 20, ambaye anatajwa kama mmoja wa makinda wanaokuja juu nchini Italia. (Corriere dello Sport via Metro)

Leeds inajiandaa kupeleka ombi la kumnasa beki wa kati wa Brazil anayekipiga Lazio, Luiz Felipe, 23
Maelezo ya picha, Leeds inajiandaa kupeleka ombi la kumnasa beki wa kati wa Brazil anayekipiga Lazio, Luiz Felipe, 23

Leeds inajiandaa kupeleka ombi la kumnasa beki wa kati wa Brazil anayekipiga Lazio, Luiz Felipe, 23. (Talksport)

Newcastle imeungana na vilabu vingine vya ligi kuu vinavyomuania mshambuliaji wa Liverpool Rhian Brewster, 20. (Chronicle)

Wawakilishi wa mlinzi wa Norway Kristoffer Ajer, 22, na kiungo wa Ufaransa Olivier Ntcham, 24, wameitaka klabu ya Celtic kutaja thamani za wachezaji hao, kabla ya kutimka. (Sky Sports)

Nahodha na mshambuliaji wa Watford Troy Deeney, 32, amewekwa sokoni kwa timu ya West Brom. (Mail

(Visited 116 times, 1 visits today)
Share this post