ASSAs

UCHEBE AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUMJERUHI SHILOLE

451
0
Share:

Mfanyabiashara Ashiraf Geuza maarufu ‘Uchebe’ amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam akikabiliwa na kosa la kumjeruhi mkewe ambaye ni msanii wa Bongo Fleva na mjasiriamali, Zuwena Mohamed maarufu ‘Shilole’ na kumsababishia maumivu.

Kwa mujibu wa taarifa, Wakili wa Jamhuri, Chesensi Gavyole ameeleza kuwa Julai 6, 2020 maeneo ya Ada Estate Kinondoni mshtakiwa alimpigia Shilole sehemu ya kichwa na shingoni na kumsababishia maumivu makali.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo amekana shtaka linalomkabili na yupo nje baada ya kukidhi masharti ya dhamana. Shauri hilo limeahirishwa hadi Septemba 23, 2020 kwa ajili ya usikilizwaji.

(Visited 62 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us