ASSAs

CARLINHOS ATAWAUWA, MIPASI KAMA DE BRUYNE, FAULO KAMA PENALTI

260
0
Share:

Maisha wa Yanga huwaelezi kitu kuhusu staa mpya, Carlos Carlinhos na jana wakamteua kuwa mchezaji bora wa mechi yao na Mbeya City ya Kocha Amri Said, ambaye ni beki wa zamani wa Simba.

Carlinhos ambaye awali baadhi ya mashabiki walikuwa na shaka na kiwango na ufiti wake, alipata asilimia 44 ya kura za mashabiki akiwashinda mastaa kibao akiwemo straika Mghana Michael Sarpong.

Kocha wa Yanga, Zlatko Krmpotic alisema Carlinhos ambaye ni mchezaji pekee wa kigeni kuwahi kupata mapokezi makubwa zaidi alipotua Bongo kuliko staa, ni mchezaji wa kiwango cha juu lakini, bado hajaiva kama inavyotakiwa licha ya kuisaidia timu yake kupata ushindi wa kwanza kwenye Ligi Kuu Bara. lakini bado hajaiva asilimia zote.

Miongoni mwa sifa za kiufundi zilizombeba Carlinhos juzi ni kupiga pasi za mbele zenye umakini, faulo za hatari, kona zenye macho na mashuti makali langoni.

Zlatko alisema Carlinhos alitumia akili, ufundi na kipaji kuamua matokeo ya mchezo huo ambao ulionekana kama Yanga inakwenda kupata sare nyingine. Katika mchezo huo baada ya kuingia dakika ya 68, Carlinhos alitengeneza nafasi zaidi ya ya tatu za kufunga, lakini wenzake walishindwa kumaliza kazi.

“Unajua Corlinhos ana uwezo na kipaji ila hakucheza mpira kwa muda mrefu kutokana na ligi kusimama kwa sababu ya corona, nahitajika kupata muda zaidi wa kumuandaa.

(Visited 49 times, 1 visits today)
Share this post