ASSAs

ERICK NAMPESYA, ANAYO FANYIWA MORRISON SIO SAHIHI

613
0
Share:

Mdau wa soka nchini Tanzania Erick David Nampesya amejitokeza hadharani na kuonesha namna alivyoguswa na tukio la kiungo mshambuliaji wa Simba SC Bernard Morrison, ambalo limechukua nafasi kubwa kwenye mitandao ya kijamii.

Morrison anashambuliwa mitandaoni kufuatia tukio la kumpiga kiwiko beki wa Ruvu Shooting Juma Nyoso, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu uliomalizika kwa Simba SC kufungwa bao moja kwa sifuri.

Nampesya ameandika kwenye ukurasa wake wa Facebook namna alivyoguswa na tukio hilo, lakini akaonyesha kumtetea Morrison ambaye kwa siku za karibuni amekua hachezi kwa kiwango cha kuridhisha kama alipokua Young Africans.

Nampesya ameandika: Soka ni mchezo wa kiungwana sana, niwe mkweli, awali sikupenda Morrison asajiliwe Simba, lakini baada ya kuwa amesajiliwa. Ninampenda Morrison kwa sababu Simba ni sehemu ya maisha yangu.

Kuhusu kitendo cha kumpiga ngumi Juma Nyosso, simtetei kama mchezaji kwa sababu hakupaswa kufanya alichofanya, ila kutokana na mfululizo wa Rafu na Vipigo, Mitama na Vifuti dhidi ya Morrison ambavyo amekuwa akitendewa huku Waamuzi wakipeta.

(Visited 188 times, 1 visits today)
Share this post