ASSAs

MGOMBEA URAIS KUPITIA CHAMA CHA ACT MAALIM SEIF AKAMATWA ZANZIBAR

298
0
Share:

Maalim Seif alikamatwa na maafisa wa polisi mapema leo katika kituo cha kupigia kura cha Garagara hatua ambayo imeshutumiwa vikali na viongozi wa upinzani. Hatahivyo polisi inadai kwamba haina taarifa zozote kuhusu kukamatwa huko kwa mwanasiasa huyo wa muda mrefu.

Kulingana na vyombo vya habari nchini humo Kamanda wa polisi mkoa wa mjini Magharibi , Awadh Juma Hajj amenukuliwa akisema kwamba hajapokea taarifa zozote za kukamtwa kwa kiongozi huyo.

Taarifa zinaarifu kwamba barabara inayoelekea katika kituo hicho imefungwa huku vitoa machozi vikirushwa.

Hatahivyo kwa mujibu wa mtandao wa twitter wa chama cha ACT Wazalendo Maalim Seif alikamatwa na vyombo vya dola wakati akiwa katika kituo cha kupigia kura cha Garagara.

(Visited 69 times, 1 visits today)
Share this post