ASSAs

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO TAREHE 11/2/2021

494
0
Share:

Kocha wa Paris St-Germain Mauricio Pochettino amesisitiza klabu yake na wachezaji hawajaonesha ”utovu wa nidhamu” kwa kuzungumzia nia yao ya kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi (ESPN)

Manchester City itamsajili mshambuliaji mpya majira haya ifanikiwe kumchua Messi au la, huku mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland, 20, akiwa kipaumbele. (90 Min)

Dortmund wanafikiria kuwauza wachezaji saba msimu huu wa joto, akiwemo winga Jadon Sancho, 20. (Mirror)

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland ni kipaumbele cha Manchester City

Kiungo wa kati wa Ubelgiji Axel Witsel,32, mshambuliaji Mmarekani Giovanni Reyna,18, kiungo wa Kiingereza Jude Bellingham,17 na Halaand ni miongoni mwa wachezaji watakaouzwa, Dortmund ikiwa imelenga kupata fedha. (Waz, via Express)

Kocha wa Chelsea Thomas Tuchel amemtaka kiungo wa kati wa PSG Kays Ruiz-Atil , 18 kumfuata Stamford Bridge. (Foot Mercato, via Team Talk)

Jose Mourinho amekiri kuwa kiungo wa Kiingereza Dele Alli, 24, yawezekana amevurugwa na uvumi unaomuhusisha yeye kuondoka Tottenham. (London Evening Standard)

Jadon Sancho ni miongoni mwa wachezaji wanaotazamiwa kuuzwa na Dortmund

Liverpool ina mpango wa kumnyakua winga wa Leeds United Raphinha,24.(France Football, via Mail)

Udinese haijaamua kumuuza kiungo wa kati Rodrigo de Paul, 26, baada ya taarifa zinazomuhusisha mchezaji huyo kuhamia Livepool wakati wa dirisha la usajili la Januari. (Goal)

West Brom wameamua kutotoa mkataba Ahmed Musa baada ya majaribio na mshambuliaji huyo wa Nigeria,28. (Express & Star)

Liverpool ina mpango wa kumnyakua winga wa Leeds United Raphinha

Kocha msaidizi wa Aston Villa John Terry yuko kwenye orodha ya watakaochukua nafasi ya kocha mkuu wa Bournemouth. (Birmingham Mail)

Kocha wa zamani wa Nice na kiungo wa kati wa zamani wa Arsenal Patrick Viera ni miongoni mwa wanaowania nafasi ya Kocha wa Bournemouth. (TalkSport)

Mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa klabu ya Strasbourg Mohamed Simakan, ambaye amehusishwa na taarifa za kuhamia Aston Villa, anajiandaa kuekelea klabu ya RB Leipzig. (Birmingham Mail)

Kocha wa Wolves Nuno Espirito Santo amesema mshambuliaji wa Mexico Raul Jimenez, 29, amepiga hatua nyingine “ya kushangaza” katika kupona kwake kutoka kwa upasuaji wa fuvu la kichwa lililovunjika mnamo Novemba. (Express & Star)

Mlinzi wa Arsenal mwenye umri wa miaka 19 Mfaransa William Saliba, ambaye anacheza kwa mkopo Nice, amemkosoa kocha wa Gunners Mikel Arteta kwa kumhukumu kwa “mechi mbili na nusu”.(ESPN)

Mshambuliaji wa Shakhtar Donetsk Manor Solomon, 21 anayehusishwa na taarifa za kuhamia Arsenal- amethibitisha kuwa vilabu kadhaa vya Primia vimeonesha nia ya kumsajili. (Goal)

Mlinzi wa Arsenal William Saliba

Tottenham na Juventus vinaelezwa kumtaka kiungo wa kati wa Sampdoria Mikkel Damsgaard, 20. (Football Italia)

Tottenham wako tayari kupanga uhamisho wa mkopo kwa ajili ya mlinzi Malachi Fagan-Walcott,18 ambaye anakipiga Dundee kwa mkopo.(Football Insider)

Barcelona kutomchezesha kiungo wa Brazil Philippe Coutinho msimu mzima ili wasiwalipe Liverpool zaidi ya euro milioni 5 (£ 4.3m) ambazo wangedaiwa ikiwa mchezaji huyo wa miaka 28 atacheza mechi tano zaidi. (Star)

(Visited 177 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us