ASSAs

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO TAREHE 18/2/2021

297
0
Share:

Bayern Munich inahofia winga wa Ufaransa Kingsley Coman, 24, huenda akashawishika kujiunga na Manchester United kwasababu ya mshahara waliotaka kumpa. (Bild, via Mail)

Arsenal inataka kumsajili kiungo wa kati wa Uhispani Dani Ceballos, 24, na mlinda lango wa Australia Mat Ryan, 28, kwa makubaliano ya kudumu msimu huu. Wawili hao sasa hivi wako Gunners kwa mkopo kutoka Real Madrid na Brighton mtawalia. (Sun)

Mshambuliaji wa Manchester United na Uruguay Edinson Cavani anataka kusalia Old Trafford kwa msimu mwingine. Mchezaji huyo, 34, alijiunga baada ya kufikiwa kwa makubaliano ya mwaka mmoja msimu uliopita. (Telegraph – subscription required)

Kylian Mbappe
Maelezo ya picha,Kylian Mbappe

Paris St-Germain imeweka euro milioni 200 kama kima wanachotaka kwa mshambuliaji wao wa Ufaransa Kylian Mbappe, 22, ambaye anafuatiliwa na Real Madrid, Liverpool, Manchester City na Juventus. (La Parisien – in French)

Mbappe anasema yuko na furaha kuwa PSG na atafanya maamuzi kwa kuzingatia malengo yake ya muda mrefu kufuatia ushindi wa Jumanne wa 4-1 dhidi ya Barcelona. (FourFourTwo)

Barcelona ingekuwa ilimsajili Mbappe mwaka 2017 lakini badala yake ikaamua kumnunua mshambuliaji wa Ufaransa, 22, Ousmane Dembele kutoka Borussia Dortmund. (Mirror)

messi

Rais wa Barcelona Joan Laporta ameahidi kufanya “kila inalowezekana” kumshawishi mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 33, kusalia katika klabu hiyo. (Sky Sports)

Real Madrid inafikiria kumsajili beki wa kati wa Villarreal raia wa Uhispania Pau Torres, 24. (Goal)

Thierry Henry na aliyekuwa mchezaji mwenza wa Arsenal Patrick Vieira wanakabiliana katika kinyanganyiro cha usimamizi Bournemouth. (Talksport)

Alexandre Lacazette
Maelezo ya picha,Mfaransa Alexandre Lacazette wa Arsenal huenda akauzwa msimu huu

Mshambuliaji wa Ufaransa Alexandre Lacazette, 29, ni mmoja kati ya wachezaji wa Arsenal ambaye huenda akauzwa msimu huu kama sehemu ya kupunguza gharama. (Sun)

Mlinzi wa Brazil David Luiz, 33, kiungo wa kati wa Uruguay Lucas Torreira, 25, na kiungo wa kati wa Ufaransa Matteo Guendouzi, 21, pia wanaoneakana kuwa tayari kuondoka Arsenal. (Star)

Atletico Madrid na mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez, 34, amesema ataamua muda muafaka wa kustaafu, lakini haitakuwa hvi karibuni. (ESPN)

Hakuna uhakika kiungo wa kati wa Uholanzi Georginio Wijnaldum, 30, atahamia Barcelona ikiwa ataondoka Liverpool kama mchezaji aliye huru, kwasababu ya masuala fedha upande wa Uhispania. (Liverpool Echo)

(Visited 103 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us