ASSAs

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO TAREHE 19/2/2021

321
0
Share:

James Rodriguez anafikiria kuondoka Everton, Chelsea inamnyatia mlinzi wa Bayern Munich, Real Madrid kuweka mkakati wa kumsajili Kylian Mbappe na mengine mengi.

Mshambuliaji wa Everton na Colombia James Rodriguez, 29, anafikiria kuondoka klabu hiyo licha ya kwamba ndio amejiunga na Goodison Park msimu uliopita. (Defensa Central – in Spanish)

Lionel Messi
Maelezo ya picha,Matumaini ya Paris St-Germain na Manchester City kumsaini Lionel Messi yafufuliwa

Manchester City imetoa ofa kwa mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi, 33, ya pauni milioni 430 kujiunga na Ligi ya Primia. Ofa hiyo inasemekana kuwa chini ya pauni milioni 600 aliyokuwa amepewa miezi sita nyuma mchezaji huyo wa Argentina ambaye hajakuwa na mkataba huko Nou Camp tangu Julai. (Sun)

Chelsea inataka kumsajili mlinzi wa Bayern Munich na Ujerumani, 25, Niklas Sule. (AZ – in German)ADVERTISEMENT

Kocha wa Chelsea Thomas Tuchel pia ameonesha nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Borussia Monchengladbach na Ujerumani Jonas Hofmann, 28. (Bild – in German)

Declan Rice

Liverpool na Manchester United wamewasiliana na ajenti wa kiungo wa kati wa West Ham Declan Rice, wakiwa na nia ya kumsajili mchezaji huyo wa Uingereza, 22, huku Chelsea ikijiondoa katika suala la uhamisho wake licha ya kwamba ni mchezaji wao. (Star)

Real Madrid inaweka mikakati ambayo itawawezesha kumpata mshambuliaji wa Paris St-Germain na Ufaransa Kylian Mbappe, 22. (AS – in Spanish)

France's Kylian Mbappe
Maelezo ya picha,Kylian Mbappe

Mbappe amepania tu kujiunga na Real Madrid au Liverpool, ikiwa ataondoka PSG msimu huu. (L’Equipe, via Mail)

Kocha wa PSG Mauricio Pochettino amesema klabu hiyo inaweza kutoa ofa kwa Mbappe kile anachotaka ili kuwa na furaha. (Catalunya Radio, via RMC Sport – in French)

Martin Odegaard
Maelezo ya picha,Martin Odegaard

Real itasitisha shughuli za kumtafuta kiungo wa kati Martin Odegaard, 22, ambaye yuko kwa mkopo Arsenal, ili kumshawishi mshambuliaji na ambaye anatoka naye nchi moja ya Norway Erling Braut Haaland, 20, kutoka Borussia Dortmund hadi Bernabeu. (Mundo Deportivo – in Spanish)

Thierry Henry huenda akathibitishwa kama kocha mpya wa Bournemouth wiki ijayo. (Mirror)

Son Heung-min, kiungo wa kati wa Tottenham raia wa Korea Kusini, amesema “sio sawa kuzungumzia mkataba mpya”. Mkataba wa sasa hivi wa mchezaji huyo, 28, unaisha mwisho wa msimu wa 2022-23. (Sun)

Juventus wanataka kumsajili tena Moise Kean
Maelezo ya picha,Juventus wanataka kumsajili tena Moise Kean

Juventus huenda ikajaribu tena kumsajili mshambuliaji wa Everton raia wa Italia Moise Kean, 20, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo PSG. Toffees ilimsajili Kean kutoka Juve mwaka 2019. (Le 10 Sport – in French)

Everton inamnyatia winga wa Real Madrid Lucas Vazquez. Winga huyo wa Uhispania, 29, pia analengwa na Napoli. (Todofichajes – in Spanish)

Chelsea huenda ikatoa ofa kwa beki wa kati Fikayo Tomori, 23, ambaye yuko AC Milan ya mkataba wa kudumu kama sehemu ya makubaliano ya mabadilishano ya kiungo wa kati wa Ivory Coast Franck Kessie, 24. Sasa hivi Tomori yuko San Siro kwa mkopo. (Il Milanista – in Italian)

Ezri Konsa
Maelezo ya picha,Ezri Konsa

Huenda Aston Villa ikatoa ofa ya pauni milioni 60 kumuuza mchezaji wa England wa Under-21 mlinzi Ezri Konsa, 23, ambaye amehusishwa na kuhamia Liverpool na Tottenham.

Aliyekuwa mshambuliaji wa Villa na England Gabby Agbonlahor amesema itakuwa ni “mara tano zaidi” pauni milioni 12 ambazo Villa ilitoa kwa Brentford kwaajili ya Konsa mwaka 2019. (Football Insider)

Norwich City imeshakubali kumpoteza beki Max Aarons kwa klabu kubwa zaidi. (Goal)

West Brom na Middlesbrough zinamnyatia mshambuliaji wa Toulouse Rhys Healey, 26. (Team Talk)

(Visited 134 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us