ASSAs

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO TAREHE 25/2/2021

477
0
Share:

Manchester City inafikiria kutoa zaidi ya £100m kuwanunua mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland, 20, na kiungo wa kati wa Marekani Giovanni Reyna, 18, mwisho wa dirisha la uhamisho . (90min)

Dortmund huenda ikakubali kumuuza Haaland mwisho wa msimu huu – mwaka mmoja kabla ya kifungu cha kandarasi yake cha dau la £70m kuanza kufanya kazi – lakini huenda ikaitisha hadi £150m. (Star)

Mshambuliaji wa Chelsea na England Tammy Abraham, 23, hayuko tayari kuingia mkataba mpya huku klabu hiyo ikiendelea kuhusishwa na Haaland. (Metro)

Tammy Abraham

Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amekiri kwamba amekuwa akiwasiliana na Haaland, ambaye alikuwa akimfunza wakati akiwa mkufunzi wa Klabu ya Molde. (Sky Sports)

Manchester United haiko tayari kulipa dau la £68m kumnunua beki wa kati wa Sevilla na Ufaransa mwenye umri wa miaka 22 Jules Kounde. (Mail)

West Ham itakabiliana na ushindani dhidi ya Leicester City iwapo wanataka kufanya uhamisho wa kiungo wa kati wa Man United Jesse Lingard 28 kuwa wa kudumu. (Express)

Jules Kounde

Manchester United inasema kwamba thamani ya Kipa wa England Dean Henderson ni £40m iwapo wataamua kumuuza mchezaji huyo. (Express)

Henderson ameendelea kufadhaishwa kutokana na ukosefu wa kushiriki mechi katika klabu hiyo ya Old. (Sky Sports)

Klabu ya Norwich City inatumai kwamba itapokea £35m kwa kumuuza beki wa England Max Aarons, 21, ambaye analengwa na Manchester United. (Metro)

Everton pia inafikiria kumnunua Aarons. (Sky Sports)

Max Aarons,

Everton haijawasiliana na Norwich kuhusu mkataba wa Aarons na inatarajia ushindani mkali kutoka kwa Manchester United, Bayern Munich na Barcelona. (Mail)

Norwich ilikaata ombi kutoka kwa Roma kumnunua beki huyo katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari. (Sun)

Beki wa Crystal Palace na Uholanzi Patrick van Aanholt ameanza mazungumzo na klabu isiojulikana iliofuzu katika ligi ya klabu bingwa. Kandarasi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 inakamilika mwisho wa msimu huu. (Football Insider)

Manchester United haitatumia kifungu cha kuongeza kandarasi ya mwaka mmoja zaidi ya kiungo wake wa kati Juan Mata 32. (MEN)

Beki wa Crystal Palace na Uholanzi Patrick van Aanholt

Klabu za ligi ya serie A Juventus, Inter Milan na Roma ziko tayari kumsaini Mata wakati atakapokuwa mchezaji huru mwisho wa msimu huu. (Sun)

Sunderland itajaribu kumsaini beki wa Wolves na England Dion Sanderson, 21, kwa kandarasi ya kudumu mwisho wa msimu. (Mail)

Tottenham inapanga kumuuza kipa Paulo Gazzaniga kwa mkataba wa kudumu mwisho wa msimu huu. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina 29 alijiunga na klabu ya Uhispania kwa mkopo mwisho wa dirisha la uhamisho la mwezi. (Football Insider)

(Visited 112 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us