ASSAs

LEO NI LEO SIMBA QUEENS NA YANGA QUEENS

600
0
Share:

Moto utawaka leo kwenye uwanja wa Uhuru saa 10:00 za jioni ambapo kutakuwa kukipigwa mechi kati ya Ligi Kuu Wanawake (WPL) kati ya wababe wawili wa ligi hiyo Yanga Princess na Simba Queens.

Mechi hiyo inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwani mpaka sasa timu zote hizo mbili hazijapoteza mchezo wa ligi hata mmoja zikiwa zimecheza jumla ya mechi 14 kwa kila mmoja.

Yanga ambao ndio vinara wa ligi hiyo yenye jumla ya timu 12, amecheza  mechi 14 akishinda 12 na kutoa sare mbili akiwa na jumla ya alama 38 kileleni huku Simba wakishika nafasi ya pili baada ya kucheza mechi 14 wakishinda 11 na kutoa sare mbili jambo linalowafanya kuwa na jumla ya alama 36.

Huu ni mchezo wa duru ya pili kwa timu hizo kukutana ambapo kwenye duru ya kwanza zilicheza Decemba 12 mwaka jana kwenye uwanja wa Mo Simba Arena na mechi hiyo kumalizika kwa suluhu (0-0). 

Mshindi wa mchezo huu ndiye atakaa kileleni mwa msimamo wa WPL, licha ya Yanga kuongoza kwa sasa lakini Simba wakishinda wataongoza kwa tofauti ya alama moja na wanajangwani hao ambao wakishinda watakuwa wamewaacha wanamsimbazi hao kwa jumla ya alama tano.

Sare yeyote katika mchezo huo haitabadili msimamo wa Ligi hiyo zaidi ya kuwaongezea nguvu vigogo hao wa kwenye WPL.

Yanga ambao ni wenyeji wa mchezo huo licha ya sasa kuonekana kuimarika wataingia uwanjani wakiwa na rekodi mbaya mbele ya Simba kwani tangu timu hiyo imeundwa haijawahi kupata ushindi mbele ya Simba na imepokea kichapo kwenye mechi zote walizokutana ukiacha ile ya awali ya msimu huu iliyomalizika kwa suluhu.

(Visited 143 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us