ASSAs

BURNA BOY NA WIZKID WASHINDA TUZO YA GRAMMY

405
0
Share:

Wasanii maarufu wa Nigeria Burna Boy na Wizkid wameshinda tuzo za Grammy za mwaka huu wa 2021.

Burna Boy ameshinda tuzo ya kipengele cha kuwa na Albamu bora ya muziki wakati Wizkid ameshinda katika kuwa na video bora zaidi kwa wimbo wake aliomshirikisha Beyoncé unaoitwa Brown Skin Girl, kutoka Lion King: Albamu ya The Gift.

Binti yake Beyoncé Blue Ivy alikuwa mshindi katika wimbo huo huo.

Katika kipengele cha video bora, tuzo inatolewa kwa msanii, muongozaji wa video na muandaaji wa video pia.

Burna Boy, ambaye jina lake halisi ni Damini Ogulu, ambaye ameshiriki kwa mwaka wa pili ameshinda katika albamu yake ya Twice As Tall .

Tuzo ya Grammy ya 63 imefanyika mjini Los Angeles. Kwa kawaida huwa sherehe kubwa ya muziki huwa inafanyika kila mwaka lakini mwaka huu hali imekuwa tofauti kutokana na janga la corona.

Hakuna watazamaji, na watumbuizaji walikuwa wametengwa katika majukwaa matano, na wakiwa kwa umbali.

Burna Boy, mwenye miaka 29, amewashinda wengine wanne ikiwemo bendi ya Malian, Tinariwen.

Wizkid
Maelezo ya picha,Albamu ya Wizkid ya Made In Lagos , ilizinduliwa mwaka 2020 ukapata mashabiki wengi

Tuzo za Grammy zimeielezea albamu ya Twice As Tall kuwa muziki uliotengenezwa kwa kiwango cha juu cha kimataifa, ni fundisho kuwa pia kwa wegine na ndio maana imemfanya Burna Boy kuingia katika kiwango hicho cha kimataifa”.

“Aliendelea kusema kuwa kuwa albam hiyo imechanganya miondoko mbalimbali kama midundo ya pop, Afrobeat, dancehall, reggae na miondoko mingine mingi,” walieleza.

Albumu yake ilishirikisha wanamuziki wengi duniani wakiwemo Stormzy, Youssou Ndour, Naughty By Nature, na Chris Martin wa Coldplay, na vilevile Sean Combs akiwa muandaaji mkuu.

Video ambayo imemfanya Wizkid kushinda imeelezewa kuwa imezingatia mitindo na kusheherekea urembo wa mwanamke mweusi mahali popote duniani “.

(Visited 81 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us