ASSAs

JE MAMA SAMIA SULUHU NI NANI?

753
0
Share:

Mama Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa Makamu wa Rais toka mwaka 2015 sasa atakuwa mrithi wa rais John Magufuli ambaye amefariki jana Jumatano Machi 17.

Samia atashikilia wadhifa huo kwa kipindi kilichosalia cha cha muhula wa urais mpaka 2025, kwa mujibu wa katiba ya Tanzania.

Anatarajiwa kuweka rekodi ya kuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo wa juu zaidi nchini Tanzania. Pia atakuwa rais wa pili wa Tanzania kutokea Zanzibar, wa kwanza akiwa Mzee Ali Hassan Mwinyi aliyeliongoza taifa hilo kwa miaka 10 kutoka mwaka 1985 mpaka 1995.

Hii pia ni mara ya kwanza kwa nchi ya Tanzania kufiwa na rais akiwa madarakani na makamu wake kuchukua nafasi.

Lakini je, Mama Samia ni nani?

TWITTER/@SULUHUSAMIA

Kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, msafara wa aliyekuwa mgombea mwenza wa CCM, Samia Hassan Suluhu, ulikuwa na wasanii wengi mashuhuri nchini.

Awali, wengi walimwogopa kwa sababu ya heshima yao kwake – lakini kuvunja mipaka, akaomba jambo moja kwao; wamwite Mama.

Tangu hapo, ukuta kati yao ukavunjika na kampeni zake zikawa na msisimko na hamasa kubwa – tofauti na ilivyozoeleka kwenye matukio ya wagombea wenza.

Kwa Watanzania wengi, jina la Samia Hassan Suluhu (60) lilipata umaarufu zaidi wakati alipoteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Katiba lililoteuliwa mwaka 2014.

Tanzania ilikuwa inaelekea kutengeneza Katiba mpya – baada ya kukamilika kwa kazi ya kukusanya maoni ya wananchi kupitia Tume ya Jaji Warioba na Mama Samia alikuwa amepewa jukumu la kuongoza mchakato huo kupitia Bunge la Katiba.

Kwa sababu bunge lile lilikuwa likionyeshwa moja kwa moja kupitia vituo mbalimbali vya runinga na Watanzania wengi wakiwa na kiu kubwa ya kujua nini kinaendelea – sura ya Samia ilianza kuzoeleka kwenye macho ya wengi na uwezo wa kuongoza ukionekana dhahiri.

(Visited 210 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us