ASSAs

KANGA ZA MAOMBOLEZI YA MAGUFULI ZAGOMBANIWA MWANZA

133
0
Share:

Wananchi wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza leo Jumatano Machi 24, 2021 wamepambana kupata kanga zenye ujumbe wa maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Magufuli katika ofisi za CCM wilayani humo.

Wananchi hao wengi wakiwa wanawake wamewataka wahusika kuwapatia za kutosha ili wazivae wakati wakimuaga kiongozi huyo aliyefariki dunia kwa ugonjwa wa moyo Machi 17, 2021.

Anna Issa amesema njia pekee ya kumuenzi Magufuli ni kuvaa kanga zenye maneno mazuri ya kumuaga.

Leo mwili wa kiongozi huyo utaagwa katika uwanja wa CCM Kirumba lakini kabla ya kufika uwanjani hapo utapitishwa maeneo mbalimbali na wananchi watapata fursa ya kumuaga huku viongozi wakiwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwa kuwa kulingana na wingi wao ni ngumu kwa kila mwananchi kupita mbele ya jeneza lenye mwili wake.

(Visited 24 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us