ASSAs

JAPAN YAIDHINISHA KUACHILIWA KWA MAJI MACHAFU NDANI YA BAHARI

43
0
Share:

Japan imeidhinisha mpango wa kuachilia zaidi ya tani milioni moja za maji machafu kutoka katika kiwanda kilichoharibiwa cha nyuklia cha Fukushima yaingie ndani ya bahari.

Maji hayo yatawekewa dawa ya kuyasafisha ili viwango vya mionzi viwe chini chini ya vile vya maji ya kunywa.

Lakini sekta ya wavuvi wa eneo hilo inapinga vikali hatua hiyo, sawa na Uchina na Korea Kusini.

Tokyo inasema kazi ya kuyachilia maji hayo yaliyokuwa yakitumiwa kupoza mafuta ya nyuklia itaanza katika kipindi cha takriban miaka miwili.

Kuidhinishwa kwa mara ya mwisho kunakuja bada ya miaka ya mjadala na unatarajiwa kuchukua miongo kumaliza.

Kiwanda cha nyuklia cha Fukushima kilipigwa na tetemeko la ardhi na tsunami mbaya ambavyo viliharibu eneo hilo na kufurika kemikali.

Kwasasa, maji ya mionzi yamesafishwa kupitia katika mchakato wa kuyachuja ili kuondoa kemikali za mionzi b, ikiwa ni pamoja na tritium – inayojulikana kama yenye madhara kwa binadamu tu pale inapowekwa kwa kiwango kikubwa.

Baadaye hutunzwa katika matanki, lakini waangalizi wa kiwanda cha Tokyo Electric Power Co (TepCo) wanasema wanaishiwa na nafasi, kwani , matanki hayo yanatarajiwa kujaa ifikapo mwaka 2022.

Takriban tani milioni 1.3 za maji ya mionzi – au yanayoweza kujaza madimbwi 500 ya Olyimpikya kuogelea – kwa sasa yametunzwa katika matanki haya, kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la habari la Reuters.

Waves breaching the sea wall of the Fukushima power plant, March 2011
Maelezo ya picha,Mwaka 2011 tsunami ilijabili bahari na kukipiga kiwanda cha Fukushima

Je kuna upinzani ?

Makundi ya mazingira kama gile Greenpeace vimekuwa vikielezea upinzani wao kwa muda mrefu dhidi ya kuachiliwa kwa maji hayo ndani ya bahari.

Shirika hilo lisilo la kiserikali (NGO) lilisema kuwa mpango wa Japan wa kuachilia maji hayo unaonesha kuwa serikali “kwa mara nyingine imewakosea watu wa Fukushima”.

Sekta ya nchi hiyo ya uvuvi pia imepinga uamuzi huo, ikihofia kwamba walaji watakataa kununua samaki waliovuliwa kutoka eneo hilo.

Sekta hiyo iliathiriwa pakubwa baada ya mkasa wa mwaka 2011, huku nchi nyingi zikipiga marufuku uagizwaji wa bidhaa za baharini kutoka kwenye mwambao wa kaskazini-mashariki mwa Japan.

Uamuzi huo umekosolewa na majirani wa Japan. Kabla ya uamuzi huo, Wizara ya mambo ya nje ya Korea Kusini Jumatatu ikielezea “kusikitika sana “.

Msemaji wa wizara mmbo ya nje ya Uchina Zhao Lijian pia aliitaka Japan “iwajibike “.

“kulinda usalama wa maslahi ya kimataifa ya umma na afya ya Watu wa China na usalama, Uchina imeelezea masikitiko yake kwa Japan kupitia mifumo ya Kidemokrasia ,”Bw Zhao alisema.

Marekani inaonekana kuunga mkono uamuzi wa Japan, hatahivyo, inaonekana kuwa na “kuidhinisha hayo kulingana na viwango vilivyokubalika vya kimataifa vya usalama wa nyuklia “.

Maji haya ni salama kwa kiwango kipi?

Japan inadai kwamba kuachiliwa kwa maji machafu ni salama kwasbabu yamesafishwa ili kuondoa katikriban mionzi yote hatari na yatachujwa sana.

Mpango huo umeungwa mkono na Shirika la Kimataifa la nguvu za atomiki , ambalo linasema kuachiliwa kwa maji hayo ni sawa na umwagaji wa maji yoyote yale machafu kutoka katika viwanda vingine kote dunaini.

“Kuachilia maji ndani ya bahari kunafanyika katika maeneo mengine duniani. Sio kitu kipya . Hakuna kashfa hapa ,” Mkurugenzi wa IAEA Director General Rafael Mariano Grossi alisema 2021.

Wanasayansi walidai kuwa iliyobakia ndani ya maji ni hatari kwa binadamu kwa dozi zinazoweza kuwa na madhara kwa binadamu kwa kiasi kikubwa wakisema kuwa kuchujwa kwa maji kunaweza kusababisha madhara ikizingatiwa kuwa hakuna ushahidi wa kisayansi unaoonesha kuwa hatari zinabainika, walisema.

Huku sumu ya mionzi ya tritium , ikiwa na uwezo wa kudumu wa miaka ipatayo 12, inamaanisha kuwa itatoweka katika mazingira kwa zaidi ya kipindi cha miongo na wala sio karne.

Mionzi inayotokana tritium inaweza kuondolewa, hatahivyo, ndio maana makundi ya sekta ya uvuvi yanahofu juu ya hatari ya kuingia kwenye maduka ya chakula na kuliwa kupitia vyakula vya baharini.

Hatari ya hili kutokea ipo, lakini muafaka wa kisayansi ni kwamba sio tisho kwa afya ya binadamu. Majaribio ya silaha yalifanywa na Marekani, Uingereza na ufaransa wakati wa miaka ya 1940 , 50 na 60.

Nini kilichotokea katika Fukushima?

tarehe 11 Machi 2011, tetemeko la ardhi la ukubwa wa 9.0 lilipiga mwambao wa kaskaini-mashariki mwa Jpan, na kusababisha tsunami ya mita 15.

Huku mifumo ya kuzuia kuyeyuka kwa nyuklia katika mtambo wa nyuklia wa Fukushima ilinusurika, uharibifu zaidi ulisababishwa na tsunami.

Huku vifaa vya kupoza mifumo vikishindwa kufanya kazi katika siku kadhaa zilizofuatia, tani za mionzi ziliachiliwa. Kuyeyuka kulikuwa ni tukio baya zaidi la nyuklia kuwahi kushuhudiwa tangu tukio la kinu cha Chernobyl mwaka 1986.

takriban watu 18,500 walikufa au kutoweka katika tetemeko hilo la ardhi na tsunami, na zaidi ya 160,000 walilazimika kuzihama nyumba zao kufuatia mkasa huo..

(Visited 8 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us