ASSAs

MISRI WADAI MAMILIONI YA DOLA KWA MMILIKI WA MELI ILIOZIBA MFEREJI WAKE MUHIMU SUEZ

43
0
Share:

Meli ya kubeba mizigo ya urefu wa takriban mita 400 kwa jina Ever Given ilikwama kimshazari katika mfereji wa Suez Machi 23 kwa karibu wiki moja na kufunga moja ya njia yenye shughuli nyingi za kibiashara duniani.

Sasa inaonekana kuwa mwisho mwema kwa Misri.

Mafanikio ya kuondoa meli hiyo iliyokuwa imekwama katika mfereji wa Suez mwisho wa mwezi Machi yalifurahikiwa kote duniani wengi wakifikiria kuwa sasa suala hilo limefika mwisho.

Lakini kinachooneka ni kwamba bado ufumbuzi wa suala hili uko mbali kupatikana.

Je hilo ni kwasababu gani? Misri imeamua kuwa haitaruhusu meli hiyo kuondoka – hadi pale itakapolipa faini ya dola bilioni moja kama fidia ya hasara iliyopatikana kipindi hicho chote cha wiki moja.

“Meli hiyo itasalia hapa hadi uchunguzi utakapokamilika na fidia kulipwa,” Osama Rabie, Rais wa Mamlaka ya Mfereji wa Suez (ACS), amearifu televisheni ya taifa nchini Misri.

Ni matumaini yetu makubaliano ya haraka tayafikiwa,” aliongeza. “Pindi tu watakapokubaliana katika suala la fidia, meli hiyo itaruhusiwa kuondoka.”

Kiwango cha fidia ya kulipwa, mwanzoni mwa Aprili Rabie alisema kuwa “hasara iliyosababishwa pamoja na gharama ya mashine iliyotumika kuirejesha meli hiyo kwenye njia yake, zote zitahesabiwa.”

“Makadirio yake yatafika dola bilioni 1 za Marekani au pengine hata zaidi kidogo. Hii ni haki ya Misri,” amesema.

Kima hiki cha pesa kitahesabiwa kulingana na ada ya usafiri iliyopoteza, hasara iliyopata wakati inatengeneza njia, juhudi za kuivuta meli hiyo na gharama za vifaa na nyenzo zilizotumika.

Shoei Kisen, kampuni moja ya Japani ambayo ndio mmiliki wa meli ya Ever Given, imesema kuwa bado haijapokea madai rasmi au ya kisheria yanayozungumzia kulipwa kwa fidia kwasababu ya hasara iliyosababishwa na kukwama kwa meli hiyo, lakini wanachojua ni kwamba wako katika mazungumzo na mamlaka inayosimamia njia hiyo ya usafirishaji.

Kwanini meli hiyo ilikwama?

Taarifa ya Osama Rabie inawadia katikati ya uchunguzi unaolenga kupata ufafanuzi wa kina kuhusu vile meli hiyo ilivyojipata ufuoni mwa mfereji wa Suez.

Sababu za awali zilizotolewa ni mawimbi makali lakini pia utafiti wa sasa unafuatilia ikiwa pengine meli hiyo ilikuwa na hitilafu za kiufundi au kibinadamu, wazo ambalo linaungwa mkono na rais wa kampuni hiyo.

“Njia hiyo haijawahi kufungwa kwasababu ya hali mbaya ya hewa,” Rabie amesema. Na pia amekanusha ya kwamba ukubwa wa meli hiyo huenda ndio chanzo.

Takriban mapipa milioni 2 ya mafuta na karibu asilimia 8 ya gesi asilia hupita katika njia hiyo ya Suez kila siku.
Maelezo ya picha,Takriban mapipa milioni 2 ya mafuta na karibu asilimia 8 ya gesi asilia hupita katika njia hiyo ya Suez kila siku.

Takriban mapipa milioni 2 ya mafuta na karibu asilimia 8 ya gesi asilia hupita katika njia hiyo ya Suez kila siku.

Pia inakadiriwa kuwa zaidi ya meli 360 zilikwama katika mfereji huo, ikiwemo kontena za kubeba mizigo, mapipa ya mafuta na gesi ya asili.

Kulingana na Osama Rabie, kukwama kwa meli kuliathiri pakubwa njia hiyo yenye shughuli chungu nzima za kibiashara gharama yake ikiwa kati ya milioni 14 na 15 za Marekani kwa kila siku iliyokuwa imekwama.

Mfereji huo ni chanzo kikuu cha mapato kwa Misri.

Hadi kabla tu ya janga la corona, biashara katika njia hiyo ilikuwa inachangia hadi asilimia 2 ya pato ghafi la ndani la nchi hiyo.

(Visited 8 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us