ASSAs

NAHODHA WA TIMU YA TAIFA YA UGANDA DENNIS ONYANGO ATANGAZA KUSTAAFU

53
0
Share:

Nahodha wa Timu ya Taifa ya Uganda The Cranes Dennis Onyango ametangaza rasmi kustaafu kucheza soka Timu ya Taifa ya Uganda akiwa na umri wa miaka 35.

Onyango anstaafu kucheza Timu ya Taifa na anabaki kuendelea kuichezea Club yake ya Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini aliyojiunga nayo 2011 akitokea Mpumalanga Black Aces ya nchini humo.

Dennis Onyango amecheza timu ya taifa ya Uganda kwa miaka 16 toka 2005 alipoitwa kwa mara ya kwanza, Onyango alizaliwa Kampala Uganda May 15 1985 na kuanza soka lake katika timu za vijana za Sharing, Nsambya na Villa SC.

2005 aliondoka Villa na kujiunga na St George ya Ethiopia (2005-2006), Super Sport United (2006-2010), Mpumalanga (2010-2011) na Mamelod Sundows 2011-hadi sasa ila 2013 hadi 2014 alienda kucheza Bidvest zote za Afrika Kusini kwa mkopo.

(Visited 6 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us