ASSAs

CHINA YAZUIA MATUMIZI YA DAWA NA CHANJO

499
0
Share:

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un alipiga marufuku utumiaji wa dawa na chanjo za China katika hospitali za mji mkuu wa Pyongyang.

Kulingana na taarifa za Asia News, kutokana na kufariki kwa afisa mwandamizi wa Korea Kaskazini baada ya kutumia dawa inayotengenezwa na China, kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-un alizuia matumizi ya dawa na chanjo dhidi zinazozalishwa China dhidi ya corona (Covid-19) katika hospitali za mji mkuu wa Pyongyang.

Hata hivyo, bado haijathibitishwa wazi iwapo dawa aliyotumia afisa mwandamizi ilisababisha kifo chake.

Wakati maafisa wa Korea Kaskazini wanadai kuwa hakuna kesi za Covid-19 nchini humo, ukweli wa madai hayo unahojiwa na mashirika ya kimataifa na jumuiya ya wanasayansi.

(Visited 161 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us