ASSAs

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO TAREHE 21/5/2021

399
0
Share:

Manchester City wako tayari kuwashinda Manchester United na Chelsea kuipata sahihi ya mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane, 27 – ambaye anasisitiza Tottenham haiwezi kumzuia kuondoka.(Star)

Wachezaji wa Spurs wanasemekana kushtushwa na uamuzi wa Kane kujitokeza kwa umma juu ya hamu yake ya kuondoka(Mirror)

Arsenal wameongeza juhudi zao za kumsajili kiungo wa Argentina mwenye umri wa miaka 24, Emiliano Buendia kutoka Norwich City inayoelekea ligi kuu wa England wakati the Gunners wakitaka kuziba nafasi ya mchezaji wa kimataifa wa Norway Martin Odegaard, 22, ambaye yuko tayari kurudi Real Madrid mwishoni mwa kipindi chake cha mkopo (Mail)

Mabingwa wa Ligi ya Premia Manchester City wamepania kumpa mshambuliaji wa England Raheem Sterling, 26, mkataba mpya wa kudumu.(Telegraph, subscription required)

Mshambuliaji wa Real Madrid wa Wales Gareth Bale, 31, anaweza kuongeza muda wake wa mkopo na Tottenham kwa mwaka mwingine ikiwa Kane atapewa ruhusa ya kuondoka klabuni humo (AS)

West Ham na Fulham wanaongoza harakati za kumsajili mshambuliaji wa Uingereza wa Blackburn Rovers, Adam Armstrong, ambaye thamani yake ni pauni milioni 25, lakini vilabu hivyo viwili vya London vinakabiliwa na ushindani kutoka kwa Brighton na Everton.(Sun)

West Bromwich Albion iko tayari kuanza mazungumzo na bosi wa zamani wa Sheffield United Chris Wilder, 53, juu ya kuchukua nafasi ya meneja anayemaliza muda wake Sam Allardyce. (Telegraph, subscription required)

Kocha wa Chelsea Thomas Tuchel bado “ana hamu sana” kumsajili beki wa Bayern Munich na Ujerumani Niklas Sule, 25. (Abendzeitung – in German)

Manchester United imeweka wazi kwa FC Nordsjaelland kwamba wako tayari kuizuia Ajax kumsajili mshambuliaji wa Ghana mwenye umri wa miaka 19 Kamaldeen Sulemana.(Football Insider)

Winga wa Wolves, Adama Traore, 25, yuko kwenye mazungumzo juu ya kandarasi mpya katika klabu hiyo ya ligi ya premia , na kukomesha uvumi unaomhusisha mchezaji huyo wa Uhispania na Liverpool na Barcelona.(Goal)

Uhamisho wa bure wa mshambuliaji wa Argentina Serio Aguero kwenda Barcelona kutoka Manchester City umekamilika kwa “80%”, huku mchezaji huyo wa miaka 32 akipangwa kufanyiwa vipimo na klabu hiyo ya Catalan mara tu baada ya City kushiriki fainali ya Ligi ya Mabingwa.(Mundo Deportivo – in Spanish)

Kipa wa Italia mwenye umri wa miaka 43, Gianluigi Buffon anasema kustaafu ni chaguo kwake wakati mkataba wake huko Turin utamalizika katika msimu wa joto, lakini anasisitiza atasaka changamoto nyingine ya “wazimu”. (Rai Sport, via Goal)

Leicester City wanakaribia kumaliza mkataba wa miaka minne wenye thamani ya jumla ya euro 25m kwa kiungo wa Ufaransa wa Lille, 22, Boubakary Soumare. (Julien Laurens on Twitter)

Newcastle United wanajiandaa kumsajili kiungo wa England wa umri wa chini ya miaka 21 Joe Willock, 21, kwa mkataba wa kudumu kutoka Arsenal, makubaliano ambayo pia yanaweza kusaidia kumshawishi winga wa Ufaransa Allan Saint-Maximin abaki St James ‘Park. (Telegraph, subscription required)

Arsenal na Tottenham zote zinavutiwa na kiungo wa Roma raia wa Gambia mwenye umri wa miaka 19, Ebrima Darboe, ambaye amecheza mara tano na klabu hiyo ya Italia (Corriere dello Sport)

Queens Park Rangers wanatarajia kumaliza makubaliano ya kumbakisha mshambuliaji wa Uingereza mwenye umri wa miaka 31 Charlie Austin baada ya kiungo wa kati wa miaka 23 Sam Field, ambaye pia alikuwa kwa mkopo kutoka klabu hiyo kukamilisha uhamisho wake wa kudumu kwenda Loftus Road. (West London Sport)

Leeds United wamepanga kutumia kifungu cha kugeuza uhamisho wa mkopo wa winga wa Uingereza Jack Harrison kutoka Manchester City kuwa mkataba wa kudumu.(Football Insider)

Uhusiano wa Wolves na Jorge Mendes utasaidia wakati kilabu hiyo ya Ligi ya Premia inapojaribu kumsajili mshambuliaji wa Ureno Goncalo Guedes kutoka Valencia, ambao “wametuma ujumbe sokoni” kusema watasikiliza ofa kwa mchezaji huyo wa miaka 24. Sevilla ni klabu nyingine imeonyesha nia ya kumtaka mchezaji huyo .(Plaza Deportiva – in Spanish)

Manchester United wako tayari kumsajili tena mlinda mlango wa Uingereza Tom Heaton mwenye umri wa miaka 35 kwa uhamisho wa bure kutoka Aston Villa. Mwingereza Sam Johnstone, 28, ambaye alikuwa mwingine aliyelengwa na na the Red Devils atahamia West Ham kutoka West Bromwich Albion(Talksport)

Chelsea na Paris St-Germain wanafikiria kumchukua kiungo wa kati wa Bosnia mwenye umri wa miaka 31 Miralem Pjanic. (Le10Sport – in French)

AC Milan mwishowe inaweza kuwa klabu ya Italia itakayomsaini mshambuliaji wa Chelsea atakayemaliza mkataba wake mwenye umri wa miaka 34 Olivier Giroud, ambaye amekuwa akifuatwa na Roma na hapo awali alikuwa akihusishwa na Lazio na Inter Milan. (Gazzetta dello Sport – in Italian)

Kocha wa zamani wa Chelsea na kiungo wa kati wa England, Frank Lampard, mwenye umri wa miaka 42, amejiondoa kwenye harakati za kuchukua nafasi ya Roy Hodgson, 73, kama meneja wa Crystal Palace msimu huu wa joto.(Football Insider)

(Visited 95 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us