ASSAs

HUSSEIN MACHOZI AJIBU MADAI YAKUWA AMEOLEWA

613
0
Share:

Msanii Hussein Machozi ameikataa kauli ya watu wanaomsema amefungiwa ndani na mwanamke nchini Italy huku wengine wakimwambia kwamba yeye ndio ameolewa na mwanamke huyo.

 Hussein Machozi amesema watanzania wanapenda sana maneno hasa wakiona mtu anaishi nje ya nchi au kupata mwanamke aliyemzidi kipato.

“Watanzania wakiona mtu amepata mwanamke mwenye pesa utaambiwa umeolewa, Ben Pol aliambiwa kaolewa na mwanamke Mkenya na Dogo Janja nae aliambiwa ameolewa na Irene Uwoya, hawajui mtu ametoka nae wapi wanasema ameolewa, mimi nilienda Ulaya kwa mambo yangu” ameeleza Hussein Machozi

“Hakuna mwanaume anayeolewa wanaume wote wanaoa, Mtanzania huwa hataki kuona mtu anafanikiwa, maneno yao huwa wanayatoa  Instagram wanaamini mtu akienda Ulaya anaenda kuishi vizuri” ameongeza

Msanii huyo amekuwa akiishi nchini Italy kwa kipindi cha miaka 7 ambapo amefanikiwa kupata mwanamke na mtoto mmoja wa kike.

(Visited 151 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us