ASSAs

JENERALI WA UGANDA ALIEPIGWA RISASI AELEZA JINSI ALIVYO NUSURIKA

478
0
Share:

Shambulio dhidi ya jenerali katumba Wamala lilifanywa na wanaume wanne ambao walikuwa kwenye pikipiki.

shambulio dhidi ya Jenerali katumba Wamala lilifanywa na wanaume wanne ambao walikuwa kwenye pikipiki.Image caption: shambulio dhidi ya Jenerali katumba Wamala lilifanywa na wanaume wanne ambao walikuwa kwenye pikipiki.

Waziri na Jenerali wa Uganda Katumba Wamala ametoa shukran zake kufuatia shambulio lililomlenga Jumanne asubuhi, akimshukuru Mungu kwa kunusurika na shambulio hilo.

Katika ujumbe alioutoa katika video fupi iliyorekodiwa kutoka katika Hospitali ya Medipal Katumba ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi amesema: ‘’Mungu amenipa nafasi ya pili . Nitakuwa vyema tena msiwe na wasi wasi , Sina majeraha mabaya, ni mikono tu, lakini nitakuwa sawa. Niko na madaktari na wanafanya kila liwezekanalo. Nawapenda nyie watu. Tafadhari muombeeni mama . Yuko katika hali mbaya’’.

Binti yake Wamala Brenda Nantongo, na dereva waliuawa katika shambulio lililofanywa na wanaume wanne ambao walikuwa kwenye pikipiki.

‘’Nimenusurika, lakini binti yangu Brenda Nantongo Katumba na dereva wangu Haruna walikufa katika eneo la tukio. Sijui sababu ya shambulio hili. Hapakuwa na sababu ya kumaliza maisha ya watu wasio na hatia. Roho zao zipumzike kwa amani’’, Ujumbe wa Twitter wa Jenerali Wamala ulisema.

Mkuu wamajeshi ya Uganda David Muhoozi alikuwa mmoja wa maafisa wa jeshi waliofika kwenye eneo la tukio mara baada ya kutokea kwa shambulio hilo, ambalo limelaaniwa vikali na Rais Yoweri Museveni.

(Visited 163 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us