ASSAs

MSANII WA MUZIKI DOGO JANJA ATAMANI BABA YAKE MZAZI ANGEKUWEPO AONE MAFANIKIO YAKE

824
0
Share:

 Nyota wa muziki wa Hip Hop nchini, msanii Dogo Janja, amesema anatamani marehemu baba yake mzazi angekuwepo hai na kushuhudia jinsi alivyobarikiwa.

Dogo Janja ambaye jina lake halisi ni Abdulaaziz Chande ameeleza hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram, ambapo ame-share picha akiwa na mpenzi wake na kuambatanisha ujumbe huo akimaanisha endapo baba yake angekuwa hai, angempa furaha zaidi mpenzi wake anayefahamika kwa jina la Quenlinna.

“Natamani marehemu baba yangu angekuepo aone how blessed he could be to have me! Ungeenjoy sana we binti,” aliandika @dogojanjatz.

Mpenzi wake huyo naye akajibu; “Usiseme hivyo hubby anatuona kila siku na nina imani tupo naye wakati wote na tushukuru Mungu tunaye mzee Jacob pia.”

@dogojanjatz kwasasa anafanya vizuri na kupitia Albamu yake mpya iitwayo ‘Asante Mama’ ambayo ni kwa ajili ya kumshukuru mama yake na wanawake wote duniani.

(Visited 168 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us