ASSAs

YOUTUBE WAMPA TUZO ZUCHU

372
0
Share:

Mtandao wa YouTube umempa Tuzo (Gold Plaque) msanii Zuchu kwa kufikisha wafuatiliaji (subscribers) Milioni 1 (1,000,000) kwenye channel yake.

Tuzo hiyo imekuwa ikitolewa kwa watoa maudhui kwenye mtandao wa Youtube ambao channel zao zinafikisha wafuatiliaji (subscribers) kuanzia 100,000 na kuendelea.

Zuchu ambaye ana mwaka mmoja na miezi miwili tangu atambulishwe rasmi kujiunga na lebo ya WCB Wasafi, Aprili 8, 2020 anakuwa msanii wa kwanza wa kike nchini kufikisha Idadi hiyo kubwa ya wafuatiliaji (1M) kwenye mtandao huo.

Anayemfuata Zuchu YouTube kwa hapa nchini ni msanii Nandy ambaye anawafuatiliaji (781K), watatu ni Christina Shusho (327K), wanne ni Rose Muhando (300K) na watano ni Vanessa Mdee (281K).

(Visited 96 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us