ASSAs

MUIMBAJI ANJELA AWEKA REKODI MPYA YOUTUBE

520
0
Share:

Mwimbaji na mwandishi wa nyimbo kutoka lebo ya muziki Konde Music Worldwide (KMW) , Anjella amejikusanyia views zaidi ya Milioni 7.97 kwenye mtandao wa YouTube kupitia maudhui (nyimbo) zake zote.

Mwimbaji huyo alijiunga na mtandao wa YouTube mwezi Oktoba 25, 2020 na amekuwa na wastani wa kutengeneza views zaidi ya milioni 1 kila mwezi kupitia kazi zake mbalimbali ambazo amezipakia kwa takribani kipindi cha miezi 7 na nusu hivi

Ikumbukwe nyota huyo wa muziki wa kizazi kipya wiki iliyopita alikabidhiwa Plaque (Silver Button Award) na mtandao wa Youtube baada ya kufikisha wafuatiliaji (Subscribers) zaidi ya  100,000

(Visited 137 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us