ASSAs

DIAMOND ATUPWA NJE TUZO ZA BET

456
0
Share:

Superstaa  Diamond Platnumz amewashukuru Watanzania wote kwa upendo waliouonesha juu yake kwenye tuzo za BET 2021 sambamba na kumuunga mkono hali inayoleta heshima kwa Tanzania.

Licha ya kukosa tuzo hiyo msimu huu, Diamond Platnumz  anaamini wakati mwingine Tanzania itatoka kimasomaso kwenye tuzo hizo.

“Kupitia tuzo hii nimeona ni kiasi gani watanzania tuna umoja, upendo na kuthamini vya kwetu. Nawashkuru sana kila mmoja wenu kwa Upendo mkubwa mlionionesha.

Nifaraja kuona Dunia inapotaja nchi zenye Wanamuziki bora Tanzania inatajwa, ni jambo la Kumshukuru Mungu. Na naamini wakati mwingine tutaibeba.

Nitafarijika kesho na kesho kutwa msanii mwingine pia akiwa katika jambo la kuwakilisha Taifa tumpe nguvu kama mlionipa. Sisi ni #SwahiliNation sisi ni Taifa la Waswahili” – Unasomeka ujumbe wa Diamond kupitia ukurasa wake wa Instagram.

(Visited 108 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us