ASSAs

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO TAREHE 9/7/2021

715
0
Share:

Paris St-Germain wanaamimi kwamba watamnasa Paul Pogba kwa bei chee ya £50m wakati huu wakiendelea kutupa ndoano zao kujaribu kumnasa kiungo huyo wa Manchester United na Ufaransa. (Star)

Liverpool imepeleka ofa kwa ajili ya kumnasa winga wa Wolves na Hispania Adama Traore, 25. (Football Insider)

West Ham inakabiliana na ushindani mkubwa kutoka kwa Atletico Madrid na Lille katika mbio za kuwania mlinda mlango wa Roma Robin Olsen. Kipa huyo wa kimataifa wa Sweden, 31, alikuwa katika kiwango bora msimu uliopita akiichezea Everton kwa mkopo na kiwango chake kwenye Euro 2020 kimewavutia wapiga nyundo hao. (AS, via West HamZone)

Hector Bellerin, 26, anataka kuondoka Arsenal na kujiunga na mabingwa wa Italia, Inter Milan. Mlinzi huyo wa pembeni mhispania alihusishwa kutimka Emirates tangu msimu uliopita na ilionekana wazi angetua Paris St-Germain. (FourFourTwo)

Meneja wa zamani wa Manchester United, Louis van Gaal, 69, anatarajiwa kumrithi Frank de Boer, 59, kama kocha mpya wa Uholanzi. (NOS)

Tottenham wanafikiria kuweka dau kwa ajili ya mlinzi anayeonekana kuja juu kutoka Wolfsburg Maxence Lacroix. Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka, 21, alijiunga na timu hiyo ya Bundesliga kutoka Sochaux msimu uliopita na amekuwa akifananishwa na Rio Ferdinand. (The Boot Room)

Winga wa Manchester United Tahith Chong anakaribia kujiunga na Birmingham kwa mkopo. Katika misimu kadhaa sasa mholanzi huyo mwenye umri wa miaka 21amekuwa akitolewa kwa mkopo kwenye vilabu vya Club Brugge ya Ubelgiji na Werder Bremen ya Ujerumani. (Telegraph)

Mshambuliaji wa Chelsea Mfaransa Olivier Giroud, 34, anakaribia kutua AC Milan ya Italia kwa mkataba wa miaka miwili. (Mail)

Mlinzi wa kulia wa Juventus Danilo, 29, ameonyesha wazi kwamba angetamani mchezaji mwenzake wa zamani wa Manchester City, Gabriel Jesus, 24, mbrazili mwenzie – kujiunga nae pale Turin, wakati huu nyota huyo akihusishwa na wakali hao wa Serie A. (Sports Illustrated)

Nyota anayewaniwa na vilabu vya Tottenham, Leeds na Leicester City Mikkel Damsgaard wa Denmark anatarajiwa kucheza ligi kuu msimu ujao, wakati huu wakala wake akianza mazungumzo na vilabu kadhaa vya England. Rais wa Sampdoria Massimo Ferrero anasema, mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 21, thamani yake imeongezeka maradufu kufuatia kiwango chake bora kwenye michuano ya Euros. (HITC)

Meneja wa Everton Rafa Benitez anamtaka mlinzi wa kifaransa Clement Lenglet, 26, kutoka Barcelona. (Fichajes)

Tottenham wanaongoza mbio za kumsaini mlinzi wa Bologna na Japan Takehiro Tomiyasu, 22. (Football Insider)

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amewatajia mabosi wa timu hiyo wachezaji watatu anaowataka msimu huu, akiwemo winga wa Ufaransa Kingsley Coman. Nyota huyo wa Bayern Munich mwenye umri wa miaka 25 anaweza kuigharimu the Reds mpaka £86m. (Mirror)

Wakati huo huo, Liverpool inamuwania pia nyota wa kimataifa wa Uholanzi Donyell Malen,22, baada ya kinda hilo la PSV Eindhoven kung’ara katika michuano ya Euro 2020. (Express)

Leeds wanajaribu kumnasa mlinzi wa Lyon na Ivory Coast Maxwel Cornet, 24. (Olympique et Lyonnais)

Kikosi hicho cha Marcelo Bielsa kinamtaka pia winga wa kiingereza Ryan Kent, 24, kutoka Rangers. (Athletic)

(Visited 97 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us