ASSAs

LINAH AMTOLEA POVU HARMONIZE BAADA YA KUMKATAA

446
0
Share:

Msanii wa muziki hapa nchini Linah Sanga amemtolea povu na kuvujisha siri nzito ya CEO wa lebo ya Konde Gang Harmonize kwa kumtaka kuwa naye kwenye mahusiano.

Linah amemchana Harmonize kupitia page yake ya Instagram kwa kuandika ujumbe ufuatao kisha kuufuta baada ya muda mfupi.

“Harmo Harmo nakuita tena, au kwa sababu sikutaki umekuwa ukinitafuta kwa njia zote nimekukataa na unakuja kwa njia huyo ya Seven kama kifua kumbe huna lolote” 

“Umeharibu familia ya wenzako leo ukaona haitoshi unakuja na kwangu, sijui hata kama ulizaliwa wewe au ulitapikwa, mwanaume una roho kama ya wanyama sikupendi nakuchukia” ameongeza

(Visited 117 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us