ASSAs

UONGOZI WA HOSPITALI YA MAWENZI WAONDOLEWA

696
0
Share:

Naibu waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel ameagiza kuondolewa kwa uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro Mawenzi, kutokana na malalamiko ya huduma mbovu katika hospitali hiyo.

Dk Mollel ametoa agizo hilo jana jioni,  wakati alipofika katika hospitali hiyo kuzungumza na watumishi, ambapo amesema uongozi wote uvunjwe na waanze na mganga mfawidhi na katibu wa hospitali.

Ameagiza pia kupewa taarifa kwa maandishi ya vituo watakapopelekwa viongozi hao, ili kuwekwe utaratibu wa kuwafuatilia kwa miezi sita ili kuhakikisha makosa waliyoyafanya Mawenzi, hayajirudii.

“Tunahitaji utawala mpya kabisa mawenzi, kuanzia Incharge (Mganga mfawidhi) hadi HMT, baada ya hapo tutafute mamangimeza wote waondoke Mawenzi na mniletee kwa maandishi fulani amekwenda wapi,fulani amekwenda wapi “amesema Dk Mollel

“Nione amepelekwa wapi asipeleke matatizo yake kule, lakini pia tumuwekee utaratibu wa yeye kufuatiliwa kila siku kwa miezi sita ili kuwa na uhakika amebadilika.”

Ameongeza kuwa “Katibu huyu atafutiwe eneo la kwenda, nimekuja hapa mara nne nikiomba wabadilike nikaomba kila mtu afanye kazi yake mara nne lakini hakuna kinachobadilika, siyo aende kuwa katibu tena kwa nafasi hii hapana, maana ameshindwa kuitendea haki hapa Mawenzi, kwa miaka yote aliyokuwepo.”

Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk Seif Shekalaghe amesema wananchi wamekuwa wakilalamikia huduma mbovu katika hospitali hiyo pamoja na baadhi ya watumishi.

“Lakini kikubwa kilichosababisha yote haya ni menejimenti ya hospitali ndiyo imefeli kusimamia ndiyo maana waziri amefanya maamuzi hayo mazito na hapa amesema ataanza na mganga mkuu mfawidhi  na katibu wake na wengine watafuata.”

(Visited 47 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us