ASSAs

LUKAKU DILI LA TIKI CHELSEA

451
0
Share:

Ingizo jipya ndani ya kikosi cha Chelsea kinachonolewa na Thomas Tuchel, Romelu Lukaku ameaza mazoezi akiwa na timu yake hiyo mpya inayoshiriki Ligi Kuu England huku akiweka bayana kwamba ni furaha kwake kurudi katika kikosi hicho.

Lukaku alijiunga na Chelsea akitokea Klabu ya Inter Milan inayoshiriki Serie A ikiwa ni mara ya pili kurejea hapo kwa kuwa awali aliuzwa 2014 kuelekea Everton.

Usajili wake kutoka Inter Milan umegharimu pauni milioni 97.5 na ni usajili wa rekodi kubwa ndani ya kikosi hicho kwa msimu huu ambao tayari umekwisha kuanza huku nchini England.

Ndani ya Inter Milan kwenye mechi 95 chini ya Kocha Mkuu, Antonio Conte msimu uliopita alifunga jumla ya mabao 64. Mazoezi ambayo wanayafanya kwa sasa ni kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu England dhidi ya Arsenal,utachezwa Uwanja wa Emirates, Jumapili na huenda nyota huyo akawa sehemu ya mchezo.

(Visited 119 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us