ASSAs

RAIS SAMIA“Prof.ELISANTE KASIMAMIE HAKI ZA KWELI ZA WATANZANIA”

311
0
Share:

NI Agosti 21, 2021 ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewaapisha viongozi wateule na miongoni aliowaapisha ni  Prof. Elisante Ole Gabriel kuwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania.

Baada ya kumuapisha aliyasema haya..”Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel kasimamie haki za kweli za Watanzania, una kazi ya kuhakikisha Magereza hayajai Watu wasio na makosa na kwamba haki inatendeka”- Rais Samia

“Kahakikishe Watumishi wa Mahakama wanafanya kazi kwa mazingira mazuri na kuangalia maslahi yao na kuhakikisha wanafanya kazi kwa nidhamu na uadilifu”-Rais Samia

“Wengine watashangaa kwanini Mmasai katolewa kwenye Ng’ombe kapelekwa Mahakamani, naamini utafanya kazi nzuri kwenye eneo hilo, kwahiyo achana na ng’ombe kwa sasa (Wizara ya Mifugo) na kashughulikie haki za Watu”-Rais Samia baada ya kuwaapisha Viongozi mbalimbali, Ikulu Dar es salaam leo”- Rais Samia

(Visited 76 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us