ASSAs

WAZIRI MKUU WA HAITI AAHIDI KUITISHA UCHAGUZI “HARAKA IWEZEKANAVYO”

180
0
Share:

Waziri Mkuu wa Haiti Ariel Henry ameahidi kuandaa uchaguzi haraka iwezekanavyo licha ya madhila yaliyosababishwa na tetemko la ardhi la wiki iliyopita kwenye taifa hilo ambalo bado limegubikwa na kiwingu cha mauaji ya rais Jovenel Moise.  Henry ameliambia Baraza Kuu la Jumuiya ya Mataifa ya kanda ya Amerika, OAS, kwamba atafanya kila kinachowezekana kuirejesha Haiti kwenye mkondo wa utawala wa kidemokrasia kwa kuandaa uchaguzi huru na wa wazi ndani ya kipindi kifupi.  Wiki iliyopita siku chache kabla ya kutokea tetemeko la ardhi lililowauwa watu 2,200, mamlaka zinazosimamia uchaguzi zilitangaza kwamba duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais iliypangwa kufanyika mwezi Septemba imesogezwa mbele hadi Novemba 7.  Inatarajiwa kuwa uchaguzi wa bunge na kura ya maoni kuhusu katiba ambavyo viliahirishwa mara mbili kutokana na janga la Covid-19 vitafanyika siku hiyo.

(Visited 33 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us