ASSAs

TETESI ZA SOKA KIMATAIFA

123
0
Share:

Real Madrid imepeleka ofa ya kwanza ya £137m kwa ajili ya mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe, 22, lakini klabu hiyo ya Ufaransa inatarajia kukataa ofa yoyote kwa ajili ya nyota huyo aliyebakiza mkataba wa mwaka mmoja. (Mail)

PSG inaweza kumuwania mshambuliaji wa Everton na Brazil Richarlison, 24, kama mbadala wa Mbappe. (Eurosport)

Mshambuliaji wa Juventus na Ureno Cristiano Ronaldo, 36, atashawishi ahamia kwa mabingwa wa ligi kuu England Manchester City katika wiki hili la mwisho la usajili, huku nyota huyo wa zamani wa Manchester United angetamani kutohitimisha mkataba wake wa mwaka mmoja uliosaliama waitalia hao. (L’Equipe – in French)

Ronaldo amezungumza kuhusu uhamisho huo na nyota wenzake wa Ureno Bernardo Silva, Ruben Dias, 24, ma mlinzi Joao Cancelo, 27. Kiungo mshambuliaji Silva au beki wa City mhispania Aymeric Laporte, wote wakiwa na miaka 27, wanaweza kujumuishwa kwenye mpango huo wa kubadilishana wachezaji. City wako tayari kulipa mshahara atakaohitaji Ronaldo, lakini hawako tayari kulipa kitita kikubwa cha ada ya uhamisho wake. (L’Equipe – in French)

Klabu za ligi kuu England Premier hazitawaruhusu wachezaji wake kuchezea timu zao za taifa katika mataifa yenye hatari kubwa ya maambukizi ya korona.

Manchester United wako katika nafasi nzuri ya kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Braut Haaland msimu ujao. Kinda huyo mwenye miaka 21 amekua lulu sokoni baada ya kufunga mabao 62 katika mechi 63 alizowachezea wajerumani hao wa ligi ya Bundasliga. (Bild – in German)

Chelsea huenda ikakabiliana na Manchester United kama watajitosa kujaribu kunasa saini ya kiungo wa Atletico Madrid na Hipsania Spain Saul Niguez, 26, kwa mkopo. (Guardian)

Kama Saul ataondoka Atletico Madrid imemuorodhesha kiungo wa Hispania Pablo Sarabia kutoka Paris St-Germain kama mbadala wake. (Marca) 

Arsenal imefanya mazungumzo na Atletico Madrid kuhusu uhamisho wa beki wa kulia wa England Kieran Trippier, ingawa beki huyo mwenye miaka 30 angetamani kwenda Manchester United kama atatakiwa kuondoka Madrid.

Washika bunduki hao hawako tayari kulipa kitita cha £34m wanacholitaka Atletico kwa ajili ya mlinzi huyo wa zamani wa Tottenham. (Eurosport)

Winga wa Brazil Willian, 33, beki wa kulia wa England Ainsley Maitland-Niles, 23, mshambuliaji wa kiingereza Eddie Nketiah, 22, mlinzi wa Hispania Hector Bellerin, 26, kiungo wa Uruguay Lucas Torreira, 25, Winga muingereza Reiss Nelson, 21, na beki wa kushoto wa and Bosnian Sead Kolasinac, 28 huenda wakatupiwa virago Arsenal wiki ijayo. (Standard)

West ham pia wana matumaini ya kumsajili mlinzi wa kati wa Ufaransa Kurt Zouma kutoka Chelsea baada ya jaribio la kumsajili mlinzi huyo mwenye miaka 26 kwenda vyema. (Telegraph – subscription required)

West Ham wanapanga kupeleka ofa kwa ajili ya mshanbuliaji wa Montpellier Gaetan Laborde, 27, lakini timu hiyo ya Ligue 1 wanaweza kuhitaji angalau £12.5m kwa ajili ya mfaransa huyo. (Le 10 Sport – in French)

West Ham wanaangalia pia uwezekano wa kumsajili winga wa CSKA Moscow na Croatia Nikola Vlasic, 23, kama mbadala wa kiungo mshambuliaji wa England Jesse Lingard, 28 kutoka Manchester United ambaye anatarajia kubaki Old Trafford. (Telegraph – subscription required)

Mawakala wa mchezaji wa kimataifa wa uholanzi Donny van de Beek, 24 wamepuuzilia mbali timu zilizoonyesha nia ya kumtaka kiungo huyo ambaye anataka kupambania namba Manchester United. (Times – subscription required)

Mlinzi wa kulia wa Liverpool na Wales Neco Williams huenda akasalia Anfield baada ya mbio za vilabu vinavyomuwania kinda huyo mwenye miaka 20 kufifia katika wiki za karibuni. (Liverpool Echo)

Ofa ya Burnley ya £15m kwa ajili ya mlinzi wa kushoto wa Ivory Coast Maxwel Cornet imekubaliwa na klabu yake ya ufaransa Lyon na sasa mpira upo kwa nyota huyo mwenye miaka 24 kama atataka kujiunga na kikosi hicho cha Turf Moor. (Sky Sports) 

Kiungo wa Uruguay Federico Valverde, 23, amekubali mkataba mpya utakaombakiza Real Madrid mpaka mwaka 2027 wneye kipengele cha malipo ya £856m kama atauzwa. (Goal)

Mlinzi wa Barcelona Sergi Roberto, 29, na kiungo mwenye umri wa miaka 33 Sergio Busquets, ambao wote ni wachezaji wa kimataifa wa Hispania wanatarajia kukubali kupunguza mishahara na kusalia kwenye klabu hiyo ya Laliga. (Marca)

(Visited 38 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us