ASSAs

NUGAZI BYE BYE YANGA

107
0
Share:

Uongozi wa klabu ya Yanga umemuaga rasmi aliyekua afisa uhamasishaji wa timu hiyo Antonio Nugaz baada ya mkataba wake kumalizika rasmi klabu hapo,Nugaz alijiunga na klabu miaka miwili iliyopita akitokea katika kituo cha habari cha Clouds

Yanga wameeleza kwenye barua yao kua wanashukuru kwa utumishi mwema aliouonyesha Nugaz kwa kipindi chote alichofanya kazi hapo.Aidha klabu imefafanua kua wameachana na Nugaz baada ya mkataba kuisha na Yanga kutoona sababu yakumuongeza mkataba mpya

Naye Nugaz ameandia haya akiwashukuru Yanga

Kwa udhati wa Moyo wangu naomba niwashukuru Kuanzia Uongozi wote wa Yanga chini ya mwenyekiti wetu Dk. Mshindo Mbette Msolla na Kaimu Katibu Mkuu Mpya Senzo Mbatha Mazingiza, wafanyakazi wenzangu wote kwa upendo wenu kwa kipindi chote cha miaka miwili niliyoitumikia @yangasc kwa moyo Mkunjufu na kujitoa kwangu, Mungu awabarik, awalinde na awape kila hitajio la nafsi zenu ili tuweze kuipeleka mbele Brand ya Yanga.

Wanachama,wapenzi na mashabiki wa Yanga ninyi mumekuwa na mimi kwa moyo mmoja Ahsanteni sana Nawapenda sana na niatendelea kuwa nanyi.

Tutaonana tena hivi Karibuni. Insha Allah.

🙏🙏🙏🙏.

(Visited 60 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us