ASSAs

MSAJILI SIJASITISHA MIKUTANO YA NDANI YA VYAMA

84
0
Share:

Msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, amekana kauli ya baadhi ya vyombo vya habari vilivyoripoti kuwa ametoa amri ya kusitisha mikutano ya ndani ya vyama vya siasa, na kuwa waliotoa taarifa hizo wamepotosha umma, iwe kwa makusudi ama kwa sababu zao binafsi.

Kupitia taarifa aliyoitoa leo Septemba 7, 2021, Jaji Mutungi amesema upotosaji huo ni kufuatia mkutano wake na waandishi wa habari alioufanya jana Septemba 6 jijini Dar es Salaam kuhusu adhma yake ya kukutana na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro pamoja na viongozi wa vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu ili kutafuta suluhu ya mivutano iliyojitokeza baina ya Jeshi la Polisi na vyama vya siasa hususani vinavyotaka kufanya makongamano na mikutano ya ndani.

Amesema, hajatoa zuio la mikutano lakini kwa busara ya kawaida aliomba, wakati jitihada hizo zinaendelea, vyama vijizuie kwa muda kuendelea na shughuli zinazosababisha kutokea kwa mivutano hiyo.

(Visited 31 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us