ASSAs

MWENDOKASI KAWE

68
0
Share:

Mradi wa mabasi ya mwendokasi mkoani Dar es Salaam, umeongeza ruti za safari za mabasi hayo na sasa umeanza kutoa huduma zake hadi Kawe.

Hii inakuja ikiwa ni siku chache tangu kuongezwe ruti ya Morocco- Mwenge iliyoanza Agosti 27, 2021 na hivyo kuwafanya wakazi wa Mwenge kuwa na ruti mbili za mabasi hayo, ukiacha ile ya Shekilango-Mwenge iliyoanza Agosti 26, 2021.

Katika ruti zote hizo nauli ni Sh400 huku ile ya Kawe ikiwa imeanza Septemba 2, 2021.

Msemaji wa wakala huo, Willium Gatambi amesema ni katika kuendelea kutoa huduma katika njia za mlisho ambazo vituo vyake vilijengwa muda mrefu.

Amesema vituo hivyo viliwekwa mahususi kwa ajili ya watu wanaotoka pembezoni mwa mji, ambapo wakifika hapo wanaunganisha usafiri wa mabasi hayo katika njia kuu

(Visited 24 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us