ASSAs

RAIA GUINEA SHANGWE KUPINDULIWA KWA RAIS ALPHA CONDE

80
0
Share:

Mamia ya raia wa Guinea wamejitokeza barabarani kuunga mkono kikosi cha makomandoo kilichomteka na kumuweka kizuizini Rais wa nchi hiyo Alpha Conde.

Kikosi hicho kinachoongozwa na Kanali Mamadi Doumbouya kimetangaza kuifuta Serikali ya nchi hiyo.

Vikosi hivyo vimetangaza kubadilisha utawala wa Magavana kwenye majimbo na kuweka utawala wa Kijeshi.

Kanali Doumbouya amesema wajibu wa Askari ni kuilinda nchi. Wanajeshi wamefunga mipaka ya nchi hiyo na kutangaza kuwa katiba ya nchi hiyo ni Batili.

(Visited 45 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us