ASSAs

SIMBA KUUMANA NA TP MAZEMBE SIMBA DAY

73
0
Share:

SASA ni rasmi Klabu ya Simba itamenyana na TP Mazembe katika mchezo wa Simba Day unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Ni Septemba 19 itakuwa kilele cha tamasha la Simba Day na Wiki ya Simba Day inatarajiwa kuanza Septemba 13.

Katika wiki hilo pia kutafanyika matukio mbalimbali ikiwa ni pamoja na usafi, kufanya matendo ya huruma kwa jamii pamoja na kununua uzi mpya wa msimu wa 2021/22 unaopatikana katika maduka ya Vunja Bei.

Siku ya kilele ni siku rasmi ya utambulisho wa wachezaji waliosajiliwa kwenye dirisha kubwa pamoja na wale waliokuwa ndani ya kikosi kwa msimu wa 2020/21.

Kwa sasa Simba imeweka kambi Arusha ikiwa na mastaa kama Bernard Morrison, Chris Mugalu, Beno Kakolanya, Gadiel Michael,  Henock Inonga na Pascal Wawa

(Visited 26 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us