ASSAs

WAZEE YANGA WAMKARIBISHA MANARA RASMI

80
0
Share:

HATIMAYE Wazee wa Klabu ya Yanga @yangasc leo Septemba 7, 2021 wamemkaribisha rasmi Msemaji wao mpya Haji Manara, ndani ya makao makuu ya timu hiyo yaliyopo mitaa ya Jangwani.

Wakiwa klabu hapo wazee wa klabu hiyo walifanya dua maalumu kwa ajili ya kuwaombea Haji Mnara pamoja na CEO wao moya Senzo Mbatha.Haji ameendelea kuwashukuru Yanga kumpatia nafasi yakua msemaji wao akiendelea kuahidi kufanya makubwa na klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya twiga na jagwani

Aidha mkuu wa kitego cha habari na mawasiliano wa klabu hiyo Hassan Bumbuli ameteta na wanahabari akiwaarifu kuhusu mchezo wao wa ligi ya mabigwa barani Afrika dhidi ya Rivers United ya nchini Nigeria utakaopigwa september 12 katika dimba la Mkapa.

Bumbuli amesema viingilio,idadi ya mashabiki watakao ruhusiwa vitawekwa wazi kesho

(Visited 37 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us