ASSAs

AZAM YAWAPIGA STOP MALIJENDARI WAKE WATATU

20
0
Share:

Uongozi wa Klabu ya Azam Umethibitisha kuwasimamisha wachezaji wake watatu waandamizi kwa muda usio na ukomo ndani ya msimu huu wa 2021/22.

Wachezaji hao ni nahodha mkuu Aggrey Morris, na wasaidizi wake, Salum Abubakar na Mudathir Yahya.

Taarifa iliyotolewa na Azam FC imeeleza kuwa sababu ya hatua hiyo ni utovu wao wa nidhamu dhidi ya meneja wa timu, Luckson Kakolaki, Septemba 18, 2021, siku ya mchezo wa pili wa raundi ya awali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Horseed SC ya Somalia

“Kabla ya mchezo walimfuata ofisini kwake na kumtamkia maneno yasiyo na staha, na baada ya mchezo wakarudia tena mbele ya wachezaji wenzao, benchi la ufundi na viongozi wote wa klabu kwenye vyumba vya kubadilishia nguo,”

“Taratibu za kinidhamu zilifuatwa ikiwa ni pamoja na kuwapatia nafasi ya kusikilizwa mbele ya kamati ya nidhamu ya klabu.
Lakini maelezo yao ya utetezi yalikosa mashiko mbele ya kamati hiyo na ndiyo maana adhabu hii inachukuliwa.” – Imeeleza Taarifa ya @azamfcofficial

(Visited 12 times, 1 visits today)
Share this post

Contact Us